Connect with us

General News

Mwanadada ashtakiwa kuiba saa na simu ya mpenziwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanadada ashtakiwa kuiba saa na simu ya mpenziwe – Taifa Leo

Mwanadada ashtakiwa kuiba saa na simu ya mpenziwe

NA RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE anayefanya biashara ameshtakiwa kwa kumwibia rafiki yake wa kiume saa na simu – vyote mali ya thamani ya Sh160,000 alipolala kwake miezi saba iliyopita.

Jackline Wanjiru Mwangi alikana mbele ya hakimu mwandamizi Derrick Kutto kwamba alimwibia Dahir Mohamud Ahmed simu na saa mnamo Novemba 2, 2021.

Wanjiru, hakimu alifahamishwa, alitiwa nguvuni baada ya kujificha miezi saba ndipo akafikishwa kortini.

Mshtakiwa alikana alimwibia Dahir na kuomba aachiliwe kwa dhamana.

Kutto alimwachilia kwa dhamana ya Sh50,000 pesa taslimu.

Kesi itasikilizwa Juni 20, 2022..