Connect with us

General News

Mwanahabari Eliud Waithaka kuzikwa Alhamisi, Machi 10 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanahabari Eliud Waithaka kuzikwa Alhamisi, Machi 10 – Taifa Leo

Mwanahabari Eliud Waithaka kuzikwa Alhamisi, Machi 10

NA MWANGI MUIRURI

JUMUIYA ya waandishi wa habari Mlima Kenya inaomboleza kifo cha Eliud Waithaka ambaye hadi mauti yake Ijumaa alikuwa akiandikia gazeti la The Star, makao yake yakiwa mjini Nanyuki.

Bw Waithaka pia ametumikia kampuni kadhaa za uchapishaji habari, ikiwemo ile ya Royal Media Services (RMS).

Alikuwa akijihusisha sanasana na habari kuhusu usalama, siasa na makala ya kuangazia masuala yanayohusu jamii katika Kaunti ya Laikipia.

Bw Waithaka alikuwa akitatizwa na afya kwa muda na taarifa kutoka kwa familia na marafiki zilisema kwamba alikumbwa na hitilafu ya kufungana pua.

“Mimi nilipigiwa simu asubuhi na rafiki yetu mwingine akiniarifu kuwa nikimbie haraka iwezekanavyo hadi nyumbani kwa Bw Eliud Waithaka kwa kuwa alikuwa amelemewa kiafya,” akasema Bw James Murimi ambaye ni mwandishi wa kampuni ya Nation Media Group katika Kaunti ya Laikipia.

Bw Murimi anasema kuwa waliabiri gari kwa dharura akiwa na waandishi wengine na kufika katika nyumba ya Bw Waithaka.

“Tulibisha mlango na akatuamkua akiwa ndani. Hakuwa amefunga mlango na ajabu ni kwamba, kufika kwa kitanda chake ambako alikuwa amelala, alikuwa haongei tena,” Bw Murimi akasema.

Aliongeza kuwa walimpeleka hadi hospitali kuu ya Nanyuki ambapo wahudumu waliompokea walitangaza kuwa alikuwa keshafariki dunia.

“Tuko katika hali ya mshangao na hatuamini kuwa huyu mtu mkarimu, mcheshi, mungwana na rafiki wa kweli ametuacha. Tulilia kuona akiandaliwa kuwekwa katika jokofu katika mochari ya Nanyuki,” akasema Bw Murimi.

Waandishi wa habari pamoja na wadau kwa sasa wamezindua harakati za kuandaa mazishi ambayo yatafanyika katika Kaunti ya Nyandarua, Alhamisi, Machi 10, 2022.