Connect with us

General News

Mwanamke abakwa na kutupwa kwa maji machafu Mukuru – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanamke abakwa na kutupwa kwa maji machafu Mukuru – Taifa Leo

Mwanamke abakwa na kutupwa kwa maji machafu Mukuru

Na SAMMY KIMATU

MWANAMKE mwenye umri wa miaka 29 aliokolewa baada ya kudaiwa kubakwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo na kuwachwa ndani ya maji machafu nje ya nyumba yake.

Kisa hiki ilitokea katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Maasai, ulioko katika tarafa ya South B, Kaunti Ndogo ya Starehe.

Kulingana na mhudumu wa masuala kuhusu dhuluma za watoto na wanawake mtaani, Bi Jane Mbula Kyalo, kisa hiki kilijawa na changamoto zake.

Bi Jane aliambia wanahabari kwamba mwathiriwa anakisiwa kutendewa unyama huo mnamo Jumapili iliyopita nyakati za usiku.

Hata hivyo, Bi Jane aliongeza kwamba mwanamke husika alidaiwa kuhamia mtaani humo kutoka mtaa jirani wa Mukuru-Kaiyaba siku mbili zilizopita.

“Inasemekana mwathiriwa alikuwa akipika na kuuza samaki mtaani jirani wa Kaiyaba alikoishi pia kabla ya kuhamia hapa mtaani wa mabanda wa Mukuru Maasai,” Bi Jane asema.

Isitoshe, Bi Jane aliongeza kwamba alijulishwa kuhusu tukio hili mwendo wa saa tano za mchana na ndipo akasimamisha shughuli zake za nyumbani ili amshughulikie mwathiriwa.

Bi Jane, akionekana kugadhabika, aliwalaumu wakazi wa mtaa wa Maasai kwa kunyamazia tukio hilo bila kuwajulisha wazee, wamama wa mtaa, viongozi wa makanisa, msikiti, maafisa wa utawala wala polisi.

“Ajabu ni kwamba wakazi wa mtaa huu hawapeani habari kuhusu uhalifu. Ni siku chache tangu kisa cha mfanyabiashara kushambuliwa na genge la majambazi waliomdunga mwanamume kisu tumboni wakimpora simu yake. Mwanamume huyo, 21 alifariki papo hapo hatua chache kutoka eneo la kisa cha leo,” Bi Jane asema.

Zaidi ya hayo ni kwamba mwathiriwa alipatikana na wamama wanaouza mboga mtaani huo mwendo wa saa tisa za asubuhi huku nao wasiwajulishe watu.

“Nilijulishwa kisa hiki mchana na mwanamke mmoja aliyepata habari kuhusu mwanamke aliyepatikana mtaani Maasai Village akilala mahali kulikuwa na matope njiani ndani ya mtaa huo,” Bi Jane akasema.

Kulingana na stakabadhi zilizopatikana ndani ya nyumba ya mwathiriwa zilionesha anatambulika kwa jina, Bi Caren Atieno, 29 (Bana jina hili)

Wahudumu wa afya waliowasili kwa ambulensi walimchukua mwathiriwa na kumpeleka hospitalini kwa matibabu.

Ndani ya nyumba ya mwathiriwa, majirani walisema huishi peke yake tangu ahamie mtaani huo.

Ndani ya nyumba yake mlikuwa na gondoro iliyotandikwa sakafuni.

Miongoni mwa vingine ni vyombo vichache ikiwemo stovu, taa aina ya koroboi, mtungi moja wa kuchotea maji wa lita kumi.

Vitu vingine vilikuwa ni sufuria moja, vikombe viwili, vijiko viwili na sahani tatu za plastiki.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending