Connect with us

General News

Mwanasiasa aponea chupuchupu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanasiasa aponea chupuchupu – Taifa Leo

Mwanasiasa aponea chupuchupu

NA WAANDISHI WETU

UCHUNGUZI umeanzishwa ili kubainisha chanzo cha kisa ambapo mwanasiasa wa Mombasa alifyatuliwa risasi 22 na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano.

Bw Ali Mwatsahu alishambuliwa mwendo wa saa nne usiku alipokuwa akiendesha gari lake karibu na JCC, Buxton.

Risasi zilifyatuliwa kutoka kwa magari mawili ambayo inaaminika yalikuwa na watu ambao walikuwa wakimfuata kisiri.

Alipata majeraha ya risasi mikononi na miguuni, akakimbizwa hospitalini ambapo anaendelea kupokea matibabu.

Kulingana na ripoti ya polisi kuhusiana na tukio hilo, walioshuhudia walisema washambulizi walikuwa wakiendesha gari dogo.

“Waliohojiwa walisema waliona gari lakini lilikuwa na nambari ya usajili isiyojulikana na walikuwa wanamkimbiza mwathiriwa,” ripoti ya polisi wa kituo cha Makupa ilisoma.

Aliyekuwa Seneta wa Mombasa, Bw Hassan Omar, ambaye ni mratibu wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA) Mombasa, alithibitisha kuwa Bw Mwatsahu amepanga kuwania kiti cha ubunge Mvita kupitia chama hicho.

“Nilimwona Bw Mwatsahu (jana Jumanne) usiku kabla hajafanyiwa upasuaji akanifahamisha kuwa ni mambo ya kisiasa. Amefanyiwa upasuaji na sasa amelazwa katika chumba cha wagonjwa. Risasi 17 zilitolewa huku tatu zikiwa tumboni hii ni kutokana na picha za CT Scan na eksirei,” akasema Bw Omar.

Mke wa pili wa mwathiriwa, Bi Mildred Odinga, alielezea kuwa mume wake alikuwa amepokea simu siku hiyo kabla ya kuondoka nyumbani.

“Mume wangu alikuwa nyumbani tukafuturu kwa pamoja. Baada ya hapo alipokea simu na kuondoka muda wa saa tatu usiku. Muda mchache baada ya hapo nikapokea simu kuwa mume wangu amepigwa risasi,” alisema Bi Odinga.

Bi Odinga aliongezea kuwa anaamini shambulio hilo lilichangiwa kisiasa.

“Waliotenda kitendo hicho ni watu ambao wanamfahamu na walijua watampata wapi na saa ngapi,” akasema Bi Odinga akiomba uchunguzi uanzishwe mara moja.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending