Connect with us

General News

Mwaniaji awataka maajenti wa UDA wawe macho mchujoni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwaniaji awataka maajenti wa UDA wawe macho mchujoni – Taifa Leo

Mwaniaji awataka maajenti wa UDA wawe macho mchujoni

Na LAWRENCE ONGARO

MAAJENTI zaidi ya 300 wa kulinda kura za mchujo za uteuzi wa ugavana Kiambu walipokea hamasisho jinsi ya kusimamia kura mnamo kesho Alhamisi.

Chama cha UDA leo kinaendesha mchujo wa kuwachagua viongozi watakaoshiriki uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina anayewania tikiti ya UDA alisem akuwa kuna upinzani mkali “mbele yangu lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu nina uhakika nitaibuka mashindi.”

Viongozi wengine ambao wamejitokeza kuwania kiti hicho cha ugavana ni seneta wa Kiambu Bw Kimani Wamatangi, na aliyekuwa gavana wa hapo awali Bw Ferdinand Waititu.

Bw Wainaina alikuwa mstari wa mbele kuwahamasisha maajenti wake jinsi ya kufuatilia uchaguzi huo.

“Nina taka kuwarai muwe chonjo kila mara mtakapokuwa katika vituo vya kupiga kura. Usikubali kutishwa na yeyote yule kwa sababu uko na haki ya kuwa katika kituo hicho,” Bw Wainaina aliwajulisha maajenti wake.

Maajenti hao walijulishwa kufika katika vituo vyao mwendo wa saa nne za asubuhi na wahakikishe wamekuwa macho hadi dakika za mwisho.

“Nyingi ndiye macho yangu katika vituo hivyo na kwa hivyo usijaribu kufunga macho hata nukta moja. Katika vituo hivyo maswala ya wizi wa kura huwa ya hali ya juu na kwa hivyo ni vyema kuwa chonjo bila kulegea,” Bw Wainaina aliwajulisha maajenti wake.

Alitoa tahadhari kwa wapinzani wake wasije kusababisha fujo Kwa kutisha maajenti wake.

“Tunaiomba serikali kufanya hima kuweka ulinzi wa kutosha katika vituo vyote vya kupiga kura,” alifafanua mbunge huyo.

Alisema wakati wa kupiga kura rejista ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC ndliyo litafuatwa kwa wapigaji kura. Kila mkazi alishauriwa kufika kituoni na kitambulisho chake ili kupiga kura.

Alisema kila kituo cha kupiga kura kitawakilishwa na maajenti wawili kwa kila mwaniaji.

Bw John Mwangi ambaye pia ni msaidizi wa mbunge huyo wa Thika, aliwahimiza maajenti hao wawe makini na wasikubali vitisho kutoka kwa mtu yeyote.

“Ukiona jambo lisilo sawa sema kwa sauti ya juu bila uwoga. Kila ajenti ana haki ya kukosoa jambo lisilo sawa kituoni” alifafanua Bw Mwangi.

Aliwashauri wazuie ujanja wa aina yoyote ambao unaweza kutokea.

“Leo nyinyi mumepewa jukumu kubwa la kushuhudia uwazi na haki. Kwa hivyo ukifanya kinyume na hivyo wewe utatajwa kama msaliti mkubwa kwa wananchi,” alifafanua Bw Mwangi.

Maajenti hao walishauriwa kuwa waaminifu kwa kazi waliyopewa na wasikubali kununuliwa na wapinzani ili kumsaliti aliyewatuma ambaye ni Bw Wainaina.