Connect with us

General News

Mwashetani aahidi kukuza vipaji vya vijana wasanii – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwashetani aahidi kukuza vipaji vya vijana wasanii – Taifa Leo

Mwashetani aahidi kukuza vipaji vya vijana wasanii

Na WINNIE ATIENO

Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani (pichani), ameahidi kukuza vipaji vya vijana kupitia sanaa.

Bw Mwashetani alisema vijana wengi wana vipawa na vipaji lakini wanapitia changamoto ya kupata soko.

Aliwasihi viongozi kukuza talanta za vijana kwa kuwasaidia na kifedha na kuwapa mwelekeo.

“Ninashukuru wale wanaokuza sanaa za vijana wetu. Kama viongozi tunafaa kuhakikisha vipaji vya vijana wetu vinaonekana na wanapata soko ili wajikimu,” alisema Bw Mwashetani.

Akiongea alipozuru studio ya Shirko Media huko Mombasa, Bw Mwashetani alisema mwaka huu wa siasa, wasanii wengi watavuna.

“Wataitwa kwenye kampeni kutumbuiza wakati wa mikutano. Vijana wenye talanta wajitokeze tuwasaidie,” aliongeza.