Connect with us

General News

Mwenye baa kuendelea na kifungo kwa kuua mpenziwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwenye baa kuendelea na kifungo kwa kuua mpenziwe

Mwenye baa kuendelea na kifungo kwa kuua mpenziwe

NA RICHARD MUNGUTI

MMILIKI wa baa mtaani Buruburu aliyemuua mpenziwe miaka minane iliyopita ataendelea kusalia ndani baada ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu kutupilia mbali ombi lake la kufutiliwa mbali kifungo cha miaka 20.

Majaji William Ouko, Wanjiru Karanja na Fatuma Sichale wa mahakama ya rufaa pamoja na James Makau walikubaliana kuhusu kifungo alichopewa Erastus Ngura Odhiambo.

Majaji hao wa Mahakama ya Rufaa walisema adhabu aliyopewa haikutosha kwa vile alimuua mpenziwe kwa njia ya kinyama.

Odhiambo aliadhibiwa kwa kumuua kinyama wakili Linda Wanjiku Irungu baada ya kukosana Desemba 2014 mtaa wa Buruburu Phase 5, Nairobi.

Ushahidi uliowasilishwa mbele ya Jaji Stella Mutuku ulisema Odhiambo alienda katika makazi ya Wanjiku lakini hakumpata.

“Mshtakiwa alimpata mpenziwe akiendesha gari na kumzuia kwa gari lake. Alimtoa Wanjiku kutoka kwa usukani wa gari lake kisha akampiga risasi na kumuua.”

Majaji walisema Odhiambo alipiga mateke maiti ya Wanjiku ishara ya kuonyesha alikusudia kumuua.

“Mshtakiwa ni miongoni mwa vijana waliotajirika na wanafurahia maisha na hawana heshima kwa maisha ya binadamu. Marehemu hakuwa na silaha lakini alitolewa garini na kuuawa kama ndege aliyetolewa kiotani,” walisema majajaji wa mahakama ya rufaa.

Jaji Makau alisema muuaji huyu hakuwasilisha ushahidi kuonyesha jinsi haki zake zimekandamizwa kwa mujibu wa Kifungu nambari 50 cha Katiba.

Mahakama hizi zilitupilia mbali maombi ya muuaji huyo na kuamuru atumikie kifungo

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending