Chifu wa eneo hilo Kennedy Wamalwa aliiambia The Standard mwanawe mchanga alipatikana akiwa angali amefungwa katika mgongo wa mamake miili hiyo ilipopatikana.
Mto Nzoia ambapo mama alijitupa na wanawe Jumapili, Julai 5 . Picha: K24 Digital. Source: UGC
“Tumekuwa tukiitafuta miili kwa siku tano. Ni afueni baada ya miili hiyo kupatikana kwani sasa polisi wataanzisha uchunguzi ili kubaini kilichompelekea mama kujitupa pamoja na wanawe mtoni,” alisema.
Kamanda wa Bungoma Kaskazini Stephen Mwoni alisema uchunguzi wa awali ulionesha kwamba mama huyo alitatizika kimawazo kufuatia ugomvi na mumewe.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.