Mwimbaji huyo amekuwa akiugua kwa muda mrefu na alikuwa akiendelea kupata nafuu nyumbani baada ya kuondoka hospitalini.
“Nilipokea simu saa tisa na dakika thelathini asubuhi ambayo ilinishtua. Ilikuwa ni simu kutoka kwa Margaret Akinyi Onyango (mamake Maureen) alikuwa analia. Nilijua mambo sio mazuri. Lady Maureen aliaga duni akiwa nyumbani kwa binamu yake eneo la Awendo. Mwili wake unapelekwa katika makafani ya Omboo,” Mike alisema.
Januari 2020, mwimbaji huyo alilazwa katika hospitali ya Pastor Machage Memoria.
Lady Maureen anatambulika kwa nyimbo maarufu kama vile Jogi Jokuoge, Alemo, Gor Kogallo, Raila miongoni mwa nyinginezo.
Kifo chake kiliombolezwa na wengi ikiwemo Kinara wa Upinzani Raila Odinga ambaye alimtaja Maureen kama mwimbaji aliyekuwa na talanta katika fani ya usanii.