Connect with us

General News

Mzee ashtakiwa kwa kuingia eneo la makaburi bila idhini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mzee ashtakiwa kwa kuingia eneo la makaburi bila idhini – Taifa Leo

Mzee ashtakiwa kwa kuingia eneo la makaburi bila idhini

Na TITUS OMINDE

MZEE mmoja alishtakiwa jana katika mahakama ya Eldoret kwa kuingia bila ruhusa katika eneo la makaburi ya familia moja eneo la Likuyani, Kaunti ya Kakamega.

Bw Peter Sirengo alishtakiwa kwa kuingia katika makaburi hayo na familia ya Bw William Ochola. Familia hiyo ilidai lengo lake lilikuwa kusumbua wafu na kusababisha fujo.Kulingana na stakabadhi ya mashtaka, Bw Sirengo aliingia katika eneo la makaburi ya familia ya Bw Ochola kinyume na sheria.

Mahakama iliambiwa kwamba mnamo Oktoba 23, katika Kijiji cha Otiende, akiwa na nia ya kumuumiza Bw Ochola kihisia, aliingia katika sehemu iliyotengewa makaburi na familia ya mlalamishi bila idhini.Bw Sirengo ambaye alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Eldoret, Bw Dennis Mikoyan, alikanusha shtaka hilo.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh10,000 pesa taslimu huku kesi hiyo ikipangiwa kusikizwa Novemba 22.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending