– Musa Otieno alilazwa kwa siku kumi katika hospitali ya Kenyatta baada ya kupatikana na virusi vya corona
– Rafiki wake wa karibu amesema kuwa mwanasoka huyo anaendelea vyema kiafya na anaamini atapona vikamilifu hivi karibuni
-Wachezaji kadhaa wa soka pamoja na Rais wa Shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa (FKF), kocha wa timu ya Harambee Stars wamemtakia Otieno afueni ya haraka
Aliyekuwa nahodha wa timu ya kitaifa ya soka Musa Otieno ameruhusiwa kuondoka hospitlani baada ya kulazwa kwa siku kumi.
Kulingana na shemeji yake Collins Okinyo, Otieno alipatikana na virusi vya COVID- 19 Juni 30, baada ya kufanyiwa vipimo.
Akithibitisha hali yake ya kiafya, rafikiye ambaye hakutaka kutambulishwa kwa majina alisema Otieno anaendelea kupata nafuu na anaamini atapona vikamilifu hivi karibuni.
Kwa sasa Otieno amejitenga na anafuata masharti yaliotolewa na wizara ya afya ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya COVID-19.
Kulingana na shemeji yake Collins Okinyo, Otieno alipatikana na virusi vya COVID- 19 Juni 30, baada ya kufanyiwa vipimo. Source: UGC
Wachezaji kadhaa wa soka pamoja na Rais wa Shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa (FKF), kocha wa timu ya Harambee Stars wamemtakia Otieno afueni ya haraka.
Wakenya wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari zinazohitajika ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivi hatari.