Polisi kaunti ya Murang’a wamemkamata Naibu Chifu mmoja na kuanzisha msako dhidi ya mwenzake na polisi waliotoweka baada ya kudaiwa kumnajisi msichana wa shule.
Watatu hao wanaripotiwa kufumaniwa msituni na wenyeji wenye hamaki wakitekeleza tendo hilo la unyama mnamo Jumatano, Julai 15 jinsi Citizen Digital ilivyoripoti.
Gari la polisi. Naibu Chifu na afisa wa polisi wasakwa baada ya kumbaka msichana wa kidayto cha tatu. Source: UGC
Machifu hao mmoja kutoka Tuthu na mwingine kutoka Wanjerere pamoja na afisa huyo wa polisi wanasemekana walimtega msichana huyo na kuingia naye msitu wa Aberdare ambapo walimnajisi.
Inasemekana ajuza mmoja aliwaona watatu hao wakiingia msituni humo na binti huyo na kuwajulisha wanakijiji ambao walianza kuwasaka.
Wenyeji hao walimnasa naibu mmoja wa chifu ambaye walimtandika kabla ya maafisa wa polisi kuwasili eneo hilo na kumkamata huku washukiwa wenzake wakitoweka vichakani.
Kamanda wa polisi John Ngare alithibitisha kisa hicho akisema kwamba uchunguzi wa kina umeanzishwa kuhusu kisa hicho.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.