Connect with us

General News

NCIC yawinda Wakenya 51 wanaoeneza chuki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

NCIC yawinda Wakenya 51 wanaoeneza chuki – Taifa Leo

NCIC yawinda Wakenya 51 wanaoeneza chuki

WINNIE ONYANDO NA WACHIRA MWANGI

TUME ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC), inachunguza watu 51 kwa kusambaza matamshi ya chuki huku kaunti sita zikitajwa kuwa huenda vurugu za kisiasa zikatokea.

Mwenyekiti wa NCIC, Samuel Kobia, alisema watu 36 walichapisha kauli za chuki kwenye mitandao ya kijamii huku wengine 15 walitoa kwenye mikutano ya kisiasa.

Alisema kuwa Kinara wa ODM, Raila Odinga na mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ni miongo – ni mwa wanasiasa wanaochunguzwa kwa madai ya kutoa matamshi yanayoaminika kuwa ya chuki.

Baadhi ya kaunti zilizotajwa kuwa huenda zikatokea vurugu za kisaiasa ni Migori, Homa Bay, Kisumu, Nandi, Kericho na Nakuru.

“Nataka kuwahakikishia Wakenya kuwa visa vyote vya matamshi ya chuki vitachunguzwa. Kila mmoja anatawaliwa na sheria kwa hivyo, hakuna aliye juu ya sheria,” akasema Dkt Kobia.

“Tumefanya kampeni za amani katika baadhi ya kaunti hizo sita. Wanasiasa wanafaa wachuje maneno yao wakifanya kampeni. Kila mmoja auze sera zake bila kuleta vurugu.”

Kadhalika, alisema kuwa tume hiyo itachapisha baadhi ya maneno ya chuki kwa lugha zote na maneno hayo kupigwa marufuku katika hafla zote za kampeni kama njia ya kudumisha amani na umoja uchaguzi unapokaribia.

Alisema kuwa baadhi ya wanasiasa wanaoendeleza matamshi ya chuki ni wale wa mirengo ya muungano wa Azimio la Umoja na Kenya Kwnza.

“Maneno kama vile ‘madoadoa’ hasa katika hafla za kisiasa inaleta utengano na chuki miongoni mwa jamii hasa zinazotoka mipakani. Vigogo vya kisiasa waepuke maneno kama hayo,”akasema Dkt Kobia.

Wakati huo huo, wawaniaji wa vyama mbalimbali eneo la Pwani wametakiwa wakumbatie amani wanaposaka kura mashinani kabla ya uteuzi kufanyika mwezi ujao.

Naibu Msajili wa vyama vya kisiasa Ali Surraw aliwataka wanasiasa wote wanaopiga kampeni kali wajiepushe na kutumia lugha ya uchochezi ambayo mara nyingi huishia kwenye ghasia.

“Tunawataka wanasiasa wae – ndeshe kampeni zao kwa kuzingatia maadili na kujiepusha na ghasia.

Uchochezi na kuzigonganisha jamii kwa misingi ya kabila haifai,” akasema Bw Surraw.

Hasa aliwataka wawaniaji ambao watapoteza kura kwenye mchujo wa vyama mbalimbali wakubali kushindwa wala wasitumie ghasia wakati wa shughuli hiyo itakayofanywa na karibu vyama vyote vikuu mwezi ujao.

Bw Surraw alikuwa akizungumza katika hoteli ya Shanzu, jijini Mombasa ambapo alikuwa akiendeleza uhamasisho kwa wawaniaji mbalimbali kuhusu stakabadhi zinazohitajika kabla ya kuwania vyeo vya uongozi.

Aidha alisema kuwa iwapo miungano mikuu ya kisiasa itasajiliwa kuwa vyama basi wawaniaji watakuwa tayari kutumia vyama hivyo kwenye nyadhifa zote sita za uongozi.

“Vyama vitakuwa vikiandaa uteuzi na vinafaa kueleza afisi ya Msajili wa vyama hasa ni siku gani ambapo watafanya uteuzi huo,” akasema Bw Surraw.

Kamishina wa Kaunti ya Mombasa Lucas Mwanza ambaye pia alihudhuria kikao hicho, aliwataka wawaniaji hao wafanye kampeni zao kwa njia ya amani.

“Tutazingatia kuwa sheria zote za kaunti zinatumika wakati wa uchaguzi. Tuandae uteuzi kwa amani na tufanye kampeni bila kuwaingilia wenzetu ambao pia wanaendeleza haki zao za kidemokrasia,” akasema Bw Mwanza.

Afisa huyo aliwataka wananchi nao waendelee na shughuli zao kama kawaida wakati wa kampeni na wawachuje viongozi kisha kuwachagua tu wale bora ambao watayazingatia maslahi yao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending