Ndege ya kijeshi imeripotiwa kuanguka katika eneo la Kathyoka kaunti ya Machakos ikiwa imewabeba maafisa wawili wa polisi ambao walikuwa wakifanyiwa mafunzo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la ndege la Marekani ndege hiyo ilianguka mwendo wa saa nne asubuhi Jumanne, Julai 13.
” Hii ilikuwa ndege iliyokuwa ikifanyiwa mafunzo, marubani wawili walikuwa kwenye ndege hiyo lakini wameweza kunusuriwa,” Taarifa kutoka wizara ya afya ilisoma.
” Leo Julai 13, ndege ya kijeshi imeanguka katika eneo la Kithyoko kaunti ya Machakos, imeripotiwa kuwa ndege hiyo ilikuwa na wanafunzi wawili waliokuwa wakifanya mafunzo,”KDF iliripoti.
Kwenye habari zingine, kamanda mkuu wa kata ndogo ya Machakos Karanja Muiruri amethibitisha kuwa waliokuwa wameabiri ndege hiyo walifariki dunia kutokana na ajali hiyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.