Connect with us

General News

Ngirita azuiliwa baada ya mdhamini wake kujiondoa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ngirita azuiliwa baada ya mdhamini wake kujiondoa – Taifa Leo

Ngirita azuiliwa baada ya mdhamini wake kujiondoa

RICHARD MUNGUTI Na WINNIE ONYANDO

MSHUKIWA mkuu katika kesi ya uwizi wa pesa za Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) Anne Ngirita, Jumanne amezuiliwa katika Gereza la Wanawake la Langata baada ya mdhamini aliyemsimamia katika kesi hiyo kujiondoa.

Tangu mwanzo, Bi Ngirita amekuwa akisimamiwa na mdhamini jambo ambalo lilimfanya aachiliwe kwa dhamana.

Haya yanajiri wiki chache baada ya chama cha Jubilee kulikataa ombi la mshukiwa huyo wa kujiunga na chama hicho ili kuwania kiti cha uwakilishi wa jinsia ya kike Kaunti ya Nakuru.

Badala yake, chama hicho kilimtaka Bi Ngirita atafute kibali kutoka kwa mashirika ya serikali kwanza kabla ya kupewa tiketi na chama hicho.

Mkurugenzi mkuu katika makao makuu ya Chama hicho, Peter Cheruiyot, ambaye alitoa taarifa hizo baada ya kumpokea Bi Ngirita na waasi wengine 20 kutoka vyama vingine, alisema kuwa viongozi wakuu wa Jubilee waliagiza kwamba Bi Ngirita anafaa kupata kibali kutoka Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai (DCI), Tume ya Maadili ya Kupambana na Ufisadi (EACC) na Mamlaka ya Ushuru ya nchini (KRA) miongoni mwa mashirika mengine kabla ya kupokelewa kama mwanachama.

“Hapo awali tulimpokea Bi Ngirita kwa chama chetu, hata hivyo, sisi kama chama tunasimamia uwazi na tunakataa ufisadi, tunataka apate kibali kutoka mashirika husika kabla ya kupewa tiketi na chama chetu,” akasema Bw Cheruyoit.

“Chama cha Jubilee kinaimarisha uongozi bora na kuhakikisha kuwa hakuna ufisadi nchini. Kwa hivyo hatutaruhusu watu walio na kesi za ufisadi kutumia tiketi ya Jubilee kuwania nyadhifa zozote katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9. Chama hakitakuwa na pa kujificha,” akaongeza Bw Cheruyoit.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending