[ad_1]
Ni raha Jamal cup ikikamilika kwa mbwembwe nairobi
Na CHARLES ONGADI
MASHINDANO ya Ndondi ya President Jamal Boxing Championsh yalikamilika kwa mbwembwe katika ukumbi wa Charter, Nairobi jumamosi huku mabondia wa Polisi wakitamba.
Klabu ya Polisi ilishinda mapigano 8 huku Majeshi ( KDF) ikishinda mapigano 5.Hata hivyo, haikuwa siku njema kwa mabondia watatu wa timu ya taifa ‘ Hit Squad ‘ waliopoteza mapigano yao kwa limbukeni.Martin Oduor wa Polisi alikuwa wa kwanza kulambishwa sakafu katika uzito wa unyoya alipoangus
hwa na Samuel Njau wa KDF naye George Cosby ( Polisi) akazabwa na Francis Denga ( Kentrack) katika uzito wa lightheavy.Katika uzito wa Cruiser, Hezron Maganga ( KDF) akashindwa na Humphrey Ochieng ( Polisi).
Katika mapigano mengine, Abednego Kyallo ( KDF) alimshinda Abdallah Charo ( Mombasa) katika uzito wa Minimum huku David Karanja ( Polisi) akimshinda Mohammed Hussein ( Kibra) katika fly.
Katika bantam, Shaffi Bakari ( Polisi) alimdengua Mwinyi Kombo ( Kongowea) huku Christine Ongare ( Polisi) akimshinda Christine Aluoch ( Siaya) katika uzito wa Minimum.Anne Wanjiru ( Kongowea) alimshinda Lencer Akinyi wa Nairobi katika light fly naye Alice Waiyego ( Nairobi ) akamshindwa na Amina Martha( Kibra) katika bantam.Beatrice Aluoch ( Nairobi)alimshinda Angela Atieno ( Nairobi) katika unyoya naye Teresiah Wanjiru ( Magereza)akamkunguta Beatrice Akinyi ( Kajiado) katika Lightwelter.
Nahodha wa timu ya taifa Nick Okoth alimshinda John Mwanzia ( G44) kwa njia ya KO katika light, Victor Odhiambo ( KDF) akamlaza Fred Onyango ( Nairobi) katika Lightwelter.Katika uzito wa welter Joseph Shigali ( Polisi) alimshinda Remmy Thiong’o ( Murang’a) katika welter huku Boniface Mogunde ( Polisi) akimnyuka Steve Olang ( Nairobi) Katika light Middle.
Katika uzito wa Middle Edwin Okong’o alipata ushindi dhidi ya Tony Hongo ( Kibra).Lorna Kusa ( Nairobi) alishindwa na Elizabeth Akinyi ( Kentrack) katika Middle huku Midia Muhatia ( KISUMU) alimnyamazisha Metrine Saginaw ( Vihiga) katika heavy.
Joshua Wasike ( Polisi) akamshinda David Njuguna ( Polisi) uzito wa heavy naye Elly Ajowi ( Polisi) akamshinda Ben Omondi ( Kentrack) katika Superheavy.
Next article
Ole Gunar Sokjaer aachishwa kazi
[ad_2]
Source link