Connect with us

General News

NIS yapewa Sh169m kwa siku, Uhuru aagiza vyombo vya usalama kuzidisha doria – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

NIS yapewa Sh169m kwa siku, Uhuru aagiza vyombo vya usalama kuzidisha doria – Taifa Leo

NIS yapewa Sh169m kwa siku, Uhuru aagiza vyombo vya usalama kuzidisha doria

Na CECIL ODONGO

SERIKALI imekuwa ikitoa Sh169 milioni kila siku kwa Idara ya Ujasusi (NIS), ripoti ya hivi punde imeonyesha.Jana, Rais Uhuru Kenyatta aliagiza vyombo vya usalama kuimarisha doria nchini.

Rais Kenyatta aliwataka maafisa wa usalama kuimarisha doria huku akisema kumekuwa na ongezeko la visa vya utovu wa usalama nchini huku kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022, zikishika kasi.

Rais Kenyatta alitoa agizo hilo baada ya kuongoza kikao cha Baraza Kuu la Usalama nchini (NSC) katika Ikulu ya Nairobi.Ripoti hiyo iliyochapishwa jana katika Gazeti Rasmi la Serikali inaonyesha idara ya NIS imepewa Sh15 bilioni kati ya Julai 1 na Oktoba 29, mwaka huu.

Hiyo ni sawa na Sh5 bilioni kwa mwezi au Sh169 milioni kwa siku. “Rais Kenyatta ameagiza asasi za usalama wa ndani kuwa macho na kuimarisha doria kote nchini,” ikasema taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kutoka Ikulu.

Idara ya NIS inayoongozwa na Bw Philip Kameru, imetengewa Sh45 bilioni kwenye bajeti katika mwaka huu wa matumizi ya fedha wa 2021/2022.Kiasi hicho kikubwa ambacho kimetengewa NIS huenda kinatokana na msimu huu wa kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022.

Kwa kawaida, wahalifu hutumia msimu wa kampeni kutenda maovu. Jumatatu, maafisa wa ujasusi walipasha habari Naibu wa Rais William Ruto kuhusu kuwepo wa njama ya kuvuruga mkutano wake Kondele, jijini Kisumu.