[ad_1]
Njonjo alidumisha maisha ya ‘kizungu’ hadi kifo
Na CHARLES WASONGA
MAREHEMU CHARLES NJONJO almaarufu Duke of Kabeteshyre, atakumbukwa kama mtu aliyekumbatia mitindo ya maisha ya hali ya juu ilivyodhihirika katika mavazi na vyakula vyake.
Hii ni kutokana na hali kwamba aliishi kwa miaka mingi nchini Uingereza ambako alisomea uanasheria. Vile vile, babaye, Josiah Njonjo, alikuwa Chifu Mkuu na hivyo alilelewa katika maisha ya anasa.
Njonjo pia alizungumza Kiingereza chenye lafudhi ya Uingereza. Alipokuwa akihudumu serikalini akiwa Mwanasheria Mkuu na Waziri, Njonjo alivaa suti nyeusi yenye virembesho vya maua ya waridi.
Suti zake zote zilikuwa za rangi nyeusi na zilitengenezwa katika kampuni moja nchini Uingereza. Ilisemekana kuwa suti zake zilikuwa zikitengenezwa mahsusi nchini Uingereza na kuwekwa nembo ya herufi za “C” na “N”, zinazoashiria jina lake; Charles Njonjo.
Vile vile, kila mara alivaa shati jeupe, mikufu ya dhahabu na tai nyeusi. Hayo ndiyo yalikuwa mavazi yake hadi alipoondoka mamlakani na uzee kumwandama.
Jinsi ilivyokuwa utotoni mwake, marafiki wa karibu wa Njonjo walikuwa wa asili ya Kizungu na Kihindi. Mmoja wao alikuwa aliyekuwa Waziri wa Kilimo Bruce McKenzie ambaye walishirikiana kuwezesha Israel kuteka uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda, 1972 na kuwakomboa raia wa nchi hiyo waliokuwa wametekwa nyara.
Ni katika mwaka huo ambapo Njonjo alimuoa Margaret Bryson akiwa na umri mkubwa wa miaka 52. Inasemekana aliamua kufunga pingu za maisha kutokana na shinikizo kutoka kwa Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
Next article
2022 ni mwaka wa kila mtu na Mola wake
[ad_2]
Source link