Connect with us

General News

Nzoia Sugar wajiondoa kutoka mduara wa kushushwa ngazi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Nzoia Sugar wajiondoa kutoka mduara wa kushushwa ngazi – Taifa Leo

Nzoia Sugar wajiondoa kutoka mduara wa kushushwa ngazi

NA JOHN KIMWERE

NZOIA Sugar ya Ligi Kuu Nchini Kenya imejiondoa kutoka mduara wa kuteremshwa daraja baada ya kudunga Posta Rangers 1-0 ugani Ruaraka, Nairobi.

Nzoia ya Bungoma ilidondosha nafasi kadhaa za wazi licha ya kutawala mchezo huo ndani ya kipindi cha kwanza. Hatua hiyo ilichangia kocha wa Posta, Salim Ali kufanya mabandiko kadhaa lakini wapi bahati haikusimama.

Kipindi cha pili mchezaji wa Nzoia alipata nafasi nzuri na kuachia kombora zito lakini mnyakaji Humphrey Katasi alikuwa ng’ang’ari. Kisha Vincent Mahiga karibu afungwe bao kabla ya kupigwa breki.

Lewis Okello wa Nzoia alikosa frikiki iliyochanjwa na Vicent Mahiga iliyompata James Kibande na kutupia kimiani bao hilo lilibakia kuwa la pekee.

Kocha Salim Ali alifanya mabadiliko tena ila nguvu mpya walishindwa kusawazisha. David Ochieng na Timothy Otieno watajilaumu vikali baada ya kupoteza nafasi za wazi.

”Tumejaribu lakini bahati haikusimama hivyo hatuna budi ila kukubali yaishe,” kocha Salim Ali alisema.

Kufuatia matokeo hayo ndani ya mechi saba, Nzoia imeshinda mara tatu na kutoka nguvu sawa mara nne. Katika jedwali la kipute hicho Nzoia imetua nafasi ya 15 kwa kuzoa alama 22, mbili mbele ya Wazito baada ya kila moja kupiga patashika 22.

Kwenye mechi nyingine, Jacob Onyango na Peter Nzuki kila mmoja alitikisa wavu mara moja na kubeba Bidco United kunyuka Mathare United mabao 2-0.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending