Connect with us

General News

OKA wakataa presha ya Uhuru – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

OKA wakataa presha ya Uhuru – Taifa Leo

OKA wakataa presha ya Uhuru

Na WANDERI KAMAU

MUUNGANO wa One Kenya Alliance (OKA) jana Jumapili ulikaidi wito wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba vinara wake wamuunge mkono kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, kuwania urais 2022.

Siku moja tu baada ya kufanya mkutano na Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi, Jumamosi, viongozi hao walionyesha msimamo mkali, wakishikilia Wakenya ndio wataamua viongozi watakaowachagua kwenye uchaguzi huo.

Wakihutubu katika kanisa la ATG Chapel, mjini Thika, Kaunti ya Kiambu, viongozi hao walisisitiza hawatakubali yeyote kuwashinikiza kumuunga mkono kiongozi fulani.

“Nyinyi wananchi ndio wenye uwezo kuwachagua viongozi wenu. Tuwache porojo za watu kujaribu kutushurutisha kwa kusema ni lazima awe huyu ama yule. Nilisema hayo nikiwa Kakamega, nitarudia nikiwa hapa na kila mahali. Uongozi hutoka kwa wananchi na lazima wafanye maamuzi yao. Kwa hivyo, chukueni kura, maanake ni nyinyi mtakaoamua yule atakayekuwa kiongozi wa nchi hii. Si viongozi wachache walioketi mahali na kufikiri wataamua wale watakaokuwa viongozi wa Kenya. Tunataka maamuzi hayo kufanywa na kila mpigakura katika kila sehemu ya kaunti zote 47,” akasema kiongozi wa ANC, Musalia Mudavadi.

Bw Mudavadi aliandamana na vinara wenzake, wakiwemo kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, Moses Wetang’ula (Ford-Kenya), Gideon Moi (Kanu) na Cyrus Jirongo.

Kwenye hafla hiyo, Bw Jirongo alisisitiza “watatoa maamuzi yao kwa Wakenya hivi karibuni” huku wenzake wakisisitiza kuhusu mikakati watakayotekeleza kufufua uchumi wa nchi.

“Siku kadhaa zijazo, tutawaeleza Wakenya mpango tulio nao kuelekea uchaguzi ujao,” akasema Bw Jirongo.

Vinara hao baadaye waliwahutubia wakazi katika maeneo ya Makongeni (Thika) na Githurai 45.

Huku kauli zao zikijiri saa chache baada ya kukutana na Rais Kenyatta, wadadisi wanasema hizo ni dalili za juhudi za Rais kutofaulu kuwarai kumuunga mkono Bw Odinga.

“Matamshi hayo yanaashiria misimamo mikali waliyo nayo viongozi hao. Ni ishara huenda juhudi za Rais hazikufaulu. Ni ukaidi wa wazi pia ikizingatiwa waliutolea katika Kaunti ya Kiambu, anakotoka Rais Kenyatta,” akasema Bw Kipkorir Mutai, ambaye ni mchanganuzi wa siasa.

Duru zilisema mkutano wa Jumamosi ndio ulikuwa sababu ya vinara hao kuahirisha mikutano kadhaa ya kisiasa waliokuwa wamepanga kufanya Ijumaa katika Kaunti ya Vihiga.

Hata hivyo, Gideon hakuhudhuria kwani alikuwa akiendesha kampeni zake katika Kaunti ya Kajiado.

Muungano huo umekuwa ukielekezwa shinikizo na wafuasi wake kumtangaza mgombea-urais wake, ikizingatiwa Naibu Rais William Ruto na Bw Odinga washaanza kuendesha kampeni zao katika sehemu mbalimbali nchini.

Kwenye mkutano uliofanyika mjini Kakamega, Alhamisi, mbunge Ayub Savula (Lugari) alisema ni wakati “viongozi hao watoke hotelini na kuanza kuvumisha azma zao sawa na vigogo wengine.”

“Wakati wa mikutano ya hoteli umeisha. Huu ni mwanzo wa msururu wa mikutano ambapo tutazuru kila mahali kukutana na Wakenya na kuwaambia ajenda tulizo nazo kufufua uchumi wa nchi,” akasema Bw Savula, ambaye pia ndiye naibu kiongozi wa ANC.

Duru zinasema baada ya mkutano wa Jumamosi, Rais anapanga kufanya kikao kingine nao na Bw Odinga.

Bw Odinga yumo ziarani Dubai kuhudhuria kongamano maalum kuhusu miundomsingi barani Afrika.

Mnamo Agosti, Rais Kenyatta alikutana na mara mbili na muungano huo pamoja na Bw Odinga, baada ya Mahakama ya Rufaa kuunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu kuharamisha Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI).

Wadadisi wanasema itamlazimu Rais Kenyatta kusuka mkakati mbadala, ikiwa lengo lake ni kuwarai viongozi hao kubuni muungano wa kisiasa kumkabili Dkt Ruto kwenye uchaguzi wa 2022.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending