Connect with us

General News

Okutoyi nje tenisi ya Santa Croce Sull’Arno nchini Italia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Okutoyi nje tenisi ya Santa Croce Sull’Arno nchini Italia – Taifa Leo

Okutoyi nje tenisi ya Santa Croce Sull’Arno nchini Italia

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Angella Okutoyi amebanduliwa kwenye mashindano ya tenisi ya J1 Santa Croce Sull’Arno nchini Italia.

Akishirikiana na Mmoroko Aya El Aouni katika mechi ya wachezaji wawili kwa wawili, Okutoyi amepoteza kwa seti mbili kavu za alama 7-6, 6-3 dhidi ya Muingereza Ranah Akua na raia wa Denmark Christine Svendsen katika raundi ya kwanza Jumatano.

Hiyo ilikuwa siku moja baada ya bingwa huyo wa Afrika mwaka 2021 na Kenya Open mwaka 2018 kuzidiwa maarifa na Aruzhan Sagandikova kutoka Kazakhstan kwa seti 2-0 za alama 6-4, 7-5 katika raundi ya 32-bora ya mechi ya mchezaji mmoja kila upande.

Kichapo cha Jumanne kilikuwa chake cha pili mfululizo katika uwanja wa udongo baada ya kupoteza dhidi ya Sandugash Kenzhibayeva 3-1 katika raundi ya pili ya J1 Casablanca nchini Morocco mwezi Machi.

Aouni pia alipoteza katika raundi ya kwanza ya mchezaji mmoja kila upande dhidi ya Mswisi Celine Naef 6-1, 6-1.

Shindano lijalo la Okutoyi ni JA Milan mnamo Mei 16-22. Anatumia mashindano hayo kujiandaa kwa mashindano ya kifahari ya Roland Garros nchini Ufaransa mnamo Mei 29 hadi Juni 5.