Connect with us

General News

Omamo ajitetea kuhusu kesi ya Miguna kurejea Kenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Omamo ajitetea kuhusu kesi ya Miguna kurejea Kenya – Taifa Leo

Omamo ajitetea kuhusu kesi ya Miguna kurejea Kenya

NA JOSEPH WANGUI

WAZIRI wa Mambo ya Nje, Raychelle Omamo, amejitetea dhidi ya madai kwamba alikaidi agizo la mahakama la kumpa Miguna Miguna hati za dharura za kusafiri mnamo Novemba mwaka jana.

Dkt Miguna anataka waziri huyo afungwe jela miezi sita kwa kudharau mahakama.

Hata hivyo, Bi Omamo alisema kuwa Dkt Miguna alikosa kufika katika ofisi ya ubalozi wa Kenya nchini Ujerumani au Canada kupewa hati hizo.

“Tangu Novemba 24, 2021, tarehe ya utoaji wa agizo hilo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ofizi za Kenya huko Berlin (Ujerumani na Ottawa (Canada) imesalia mikononi mwa Dkt Miguna lakini

hajarejea kutafuta hati za dharura za usafiri,” akasema Bi Omamo kwenye karatasi za mahakama. Dkt Miguna alijulisha korti kuwa Bi Omamo alikataa kutii agizo la korti lililotolewa na hakimu mwandamizi, Hedwig Ong’undi.

Kupitia wakili Kamotho Njenga, Dkt Miguna alisema kuwa balozi hiyo ilimyima hati za kusafiri.

Mnamo Novemba 25, baada ya kungoja kwa zaidi ya saa 96 jijini Berlin, alisafiri kurejea Toronto, Canada. Waziri Omamo alisema Dkt Miguna alipoenda kwa ubalozi huo, Wizara na Mwanasheria Mkuu hawakuwa wamepewa amri ya mahakama.

Alisema aliarifiwa kuhusu agizo la mahakama na Mwanasheria Mkuu, Kihara Kariuki mnamo Novemba 24.