Connect with us

General News

Pembejeo ghali kupunguza ukuzaji mahindi Bondeni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Pembejeo ghali kupunguza ukuzaji mahindi Bondeni – Taifa Leo

Pembejeo ghali kupunguza ukuzaji mahindi Bondeni

Na BARNABAS BII

BEI za juu za mbolea na mbegu zimefanya wakulima wengi katika eneo la onde la Ufa kupunguza mashamba wanayopanda mahindi jambo linalotishia utoshelevu wa chakula nchini.

Ingawa bei ya mbolea hutegemea soko, mfuko wa kilo 50 wa mbolea aina ya DAP unauzwa kwa Sh5,200 kutoka Sh3,500 eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Wakulima wanasema huenda wakalazimika kupanda mimea bila kutumia mbolea kutokana na kupanda kwa bei ya mbolea hatua itakayoathiri mazao.

“Hatuna la kufanya isipokuwa kupunguza eneo tunalopanda nafaka ili kupunguza gharama kufuatia kuongezeka kwa bei za mbolea na mbegu za mahindim,” alisema.

Jackson Kosgey kutoka Moiben kaunti ya Uasin Gishu.Kampuni ya Kenya Seed imeongeza bei ya mbegu za mahindi hadi Sh4,700 kutoka Sh4,500 kwa pakiti ya kilo 25.

“Inakuwa vigumu kumudu gharama ya juu ya uzalishaji huku bei za zao zikishuka ishara ya hali ngumu kiuchumi kwa wakulima wa mahindi,” alisema.

Eliud Kibet, mkulima kutoka Kerita, Kesses kaunti ya Uasin Gishu.Haya yanajiri huku wizara ya kilimo ikionya kuwa nchi itakubwa na uhaba wa mahindi baada ya Machi 2022.

Hii itafanya bei ya unga wa mahindi kupanda. Wakulima wamekataa kuuza mahindi wakisubiri bei ziimarike.

Kwa sasa, ushindani umezuka kati ya serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Mazao na Nafaka na kampuni za kusaga unga na kufanya bei ya gunia la kilo 90 la mahindi kuwa Sh3,000.