[ad_1]
Pesa za kampeni zawagonganisha washirika wa Ruto
NA PIUS MAUNDU
WASIWASI umewakumba wafuasi wa Naibu Rais William Ruto katika kaunti ya Makueni baada ya mirengo miwili ya viongozi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kuchipuka.
Taifa Leo imebaini kuwa mgawanyiko huo umesababishwa na vita vya ubabe miongoni mwao na usambazaji wa mamilioni ya fedha za kufadhili kampeni za Dkt Ruto.
Tofauti zilitokea baada ya mwenyekiti wa UDA Johnstone Muthama kumteua Emmanuel Mutisya kuwa kiongozi wa kampeni za Dkt Ruto katika eneo hilo na kumpa mamlaka ya kusimimia fedha za kampeni.
Hatua hii ilikasirisha kundi jingine la wandani wa Dkt Ruto wanaojulikana kama Super Six ambalo liliwakashifu Bw Muthama na Profesa Mutisya kwa kuendeleza “udikteta ndani ya UDA.”
Wanachama wa kundi la Super Six wanajumuisha aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Michezo Nchini Fred Muteti, aliyekuwa mkurugenzi wa NEMA Terry Mbaika, aliyekuwa mbunge wa Kilome Ragina Ndambuki na wafanyabiashara James Mbaluka, Amos Ngumbi na Onesmus Kimilu.
Wafanyabiashara hawa wanamezea mate viti mbalimbali katika kaunti ya Makueni.
Kundi la pili la wagombeaji linalojumuisha waliokuwa wabunge wa Kaiti Gideon Ndambuki na Richard Makenga wanamuunga mkono Profesa Mutisya ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha ugavana katika kaunti hiyo.
Makundi haya mawili huandaa mikutano sehemu tofauti ambako wao hurushiana cheche za maneno badala ya kumpigia debe Dkt Ruto, chama cha UDA au kujipigia debe kwa viti wanavyotaka kuwania.
Wanachama wa kundi la Super Six wamewashangaza wafuasi wa UDA katika kaunti ya Makueni kwa kumfanyia kampeni waziwazi Seneta wa Makueni
Next article
Jumwa abanwa katikati ya ndume
[ad_2]
Source link