[ad_1]
Pigo kwa Chelsea beki Chilwell sasa akitarajiwa kukosa mechi zote za kampeni za msimu huu
Na MASHIRIKA
DIFENDA Ben Chilwell wa Chelsea sasa atakosa mechi zote zilisosalia katika kampeni za msimu huu wa 2021-22 baada ya waajiri wake kuthibitisha kwamba atafanyiwa upasuaji wa goti wiki ijayo.
Beki huyo wa kushoto raia wa Uingereza alipata jeraha baya alipoongoza Chelsea kutandika Juventus 4-0 katika mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Novemba 23, 2021.
Kufikia sasa, nyota huyo wa zamani wa Leicester City amefungia Chelsea mabao matatu na kuchangia sita mengine katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu.
Ingawa madaktari wa Chelsea walipania kumtibu Chilwell bila kumfanyia upasuaji, pendekezo la utaratibu huo kutekelezwa limeidhinishwa baada ya jeraha lenyewe kutopona jinsi ilivyotarajiwa.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
Salah, Elneny na Trezeguet kuongoza Misri katika fainali za…
[ad_2]
Source link