Connect with us

General News

Polisi asema atamlipa aliyeumwa na mbwa Sh150 pekee si elfu 32 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi asema atamlipa aliyeumwa na mbwa Sh150 pekee si elfu 32 – Taifa Leo

Polisi asema atamlipa aliyeumwa na mbwa Sh150 pekee si elfu 32

Na MWANGI MUIRURI

MKUTANO wa kujaribu kuleta maridhiano kati ya afisa wa polisi na raia uliishia kuwa vurugu baada ya afisa huyo kusema angemlipa mhasiriwa Sh150 tu kwa kumsababishia kuumwa na mbwa wa polisi.

Konstebo wa Polisi, Lucy Nyambura anashutumiwa kwa kuachilia mbwa wa polisi aliyemuuma Bw Julius Mburu mwenye umri wa miaka 31.

Afisa huyo alisisitiza kuwa mbwa wake amepokea chanjo zote hivyo basi hakuna hatari ya kumwambukiza mhasiriwa ugonjwa wowote.

Alihoji kuwa Bw Mburu alihitaji tu kufungwa kidonda chake mara tatu kwa gharama ya Sh50 kila moja.

Katika madai yake ya maridhiano, Bw Mburu alitaka kurejeshewa Sh5,000 atakazotumia kupokea chanjo za kuzuia kichaa cha mbwa, Sh14,000 kugharimia mapato atakayopoteza kwa wiki mbili akiugua, Sh3,000 za usafiri hadi hospitalini na Sh10,000 kufidia kudhalilishwa na hofu aliyopitia, zote zikiwa Sh32,000.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending