Connect with us

General News

Polisi lawamani kwa kukosa kuzima mauaji ya wakongwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi lawamani kwa kukosa kuzima mauaji ya wakongwe – Taifa Leo

Polisi lawamani kwa kukosa kuzima mauaji ya wakongwe

KILIFI

Na MAUREEN ONGALA

MBUNGE wa Rabai, Bw William Kamote, amelalama kuwa utepetevu wa polisi ndio unachangia ongezeko la mauaji ya wakongwe kwa tuhuma za uchawi, katika Kaunti ya Kilifi.

Alisema uzembe huo umewapatia washukiwa nguvu huku maswali mengi yakiendelea kuulizwa kuhusiana na mauaji ya watu 20.Malalamishi ya Mbunge huyo yanajiri wakati ambapo Naibu Kamishna wa Kaunti anayesimamia kaunti ndogo ya Rabai, Bw Musa Issa, kuamuru mauaji yote katika eneo hilo yachunguzwe.

Kaunti hiyo ndogo imeandikisha ongezeko la visa vya wakongwe kuuawa kwa tuhuma za uchawi.Akiongea katika mkutano wa usalama eneo la Bwagamoyo, wadi ya Mwawesa, Bw Issa, alisema sharti wanajamii waelezee kiini cha vifo vyote.

“Visa vyote vya mauaji vitaendelea kuchunguzwa hadi tutakapowakamata wahusika wote. Sharti tuwajibikie kila mtu aliyeuawa Rabai. Sharti tuwasake wahusika wote,” akasema.Alieleza kuwa aliwahi kutembelea familia ya mmoja wa wakongwe waliouawa, akiandamana na maafisa wa polisi lakini akashangaa kuwa vijana wote katika eneo hilo hawakuwepo walipowasili.

“Hali katika boma hilo litaibua maswali mengi kwa mpelelezi yeyote,” akaeleza.Bw Issa pia aliongeza kuwa familia katika eneo hilo, hazifuatilii visa hivyo vya mauaji ya wakongwe, hali inayoashiria kuwa watu wa familia ndio wahusika katika mauaji hayo.

“Haileweki ni kwa nini mpendwa wako ameuawa, uchunguzi unaendelea lakini kama familia hamjawahi kufuatilia kujua uchunguzi huo umefikia wapi,” akasema.Alisema anashauriana na wazee na viongozi wa kidini katika eneo bunge hilo la Rabai kuhusiana na suala hilo.Lakini Bw Kamoti alielekeza lawama kwa maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai (DCI) eneo hilo kwa utepetevu.

Mbunge huyo alisema zaidi ya visa 20 vya mauaji havijashughulikiwa na wahusika kutiwa mbaroni.Kata ndogo ya Bwagamoyo pekee imeandikisha jumla ya visa 18 vya mauaji hayo tata.“Watu wa familia hukamatwa hata kabla ya maafisa wa polisi kupeleka mwili katika hifadhi ya maiti.

Lakini tunataka matokeo ya uchunguzi.” Akaongeza, “Haiwezekani kwamba hakuna haya mtu mmoja amekamatwa na kushtakiwa kortini kuhusiana na mauaji ya watu hawa 18.”Bw Kamoti pia alisema kuwa hali hiyo imeibua hofu miongoni mwa wakazi wengi hata wakiogopa kutoka nje wasije wakashambuliwa.

Vilevile, alisema maafisa wa DCI wamefeli kuelezea ni kwa nini wahusika hawajakamatwa ili wafunguliwe mashtaka.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending