Connect with us

General News

Polisi Rabai wasema sababu za kihistoria zinachangia mauaji eneo hilo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi Rabai wasema sababu za kihistoria zinachangia mauaji eneo hilo – Taifa Leo

Polisi Rabai wasema sababu za kihistoria zinachangia mauaji eneo hilo

NA MAUREEN ONGALA

UOZO wa baadhi ya maafisa wa polisi umeibuka tena, baada ya mwanamke mkongwe kutoka Kaunti ya Kilifi kulalamika kuitishwa Sh4,000, alipopiga ripoti kituoni kwamba mwanawe alitaka kumuua.

Bi Dama Mlonzi, 70, ambaye ni mjane, alilazimika kutoroka nyumbani kwake mwezi Februari akihofia maisha yake yalikuwa hatarini kuhusu mzozo wa ardhi, huku baadhi ya watoto wake pia wakimsingizia ni mchawi.

Kulingana naye, mwanawe alianza kumtishia 2018, miaka michache tu baada ya mumewe kufariki. Kisa na maana ni hatua yake ya kuuza kipande cha ardhi ili apate pesa za kujijengea nyumba nadhifu.

Mama huyo wa watoto tisa alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Kilifi angalau kupata ulinzi.Badala yake, anadai maafisa polisi walimuitisha pesa za mafuta ambazo hakuwa nazo.

“Waliniambia nirudi nyumbani nitafute pesa kisha niende kutafuta usaidizi katika kituo cha polisi cha Ngerenya,” alieleza Taifa Leo.

Alipoona vitisho vimezidi, aliamua kupiga ripoti katika kituo cha Ngerenya lakini hapo pia hakusaidiwa.

“Polisi waliniambia nitafute Sh4,000 za kuwezesha kukamatwa kwa mwanangu, lakini sijafanikiwa kupata pesa hizo,” akasema.

Bi Dama Mlonzi (kati), nduguye mdogo Bw Jocktan Charo pamoja na mkewe Bi Euince Jumwa katika boma lao eneo la Makusheni kwenye Wadi ya Kibarani, Kaunti ya Kilifi. PICHA | MAUREEN ONGALA

Mkuu wa Polisi katika Kaunti Ndogo ya Kilifi Kaskazini, Bw Jonathan Koech, aliwataka maafisa kukoma kuitisha pesa kabla kuhudumia umma.

Alithibitisha kwamba mshukiwa aliyedaiwa kutishia maisha ya mamake alishakamatwa Jumapili baada ya malalamishi kufika katika afisi yake, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi punde.

“Sio vizuri polisi kuitisha pesa ndipo wasaidie wananchi. Tuwe tayari kufanya kazi,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa maafisa sasa wako katika harakati za kuandaa faili za kesi ya mshukiwa kisha apelekwe mahakamani.

Wazee wengi katika kaunti za Kilifi na Kwale wamekuwa wakiishi katika hofu kwani jamaa zao hudai ni wachawi, kabla kupanga njama za kuwaua; hii ikiwa kisingizio chao kupata nafasi ya kurithi mashamba ya wahasiriwa.

Wiki iliyopita, mzee mwenye umri wa miaka 67 kutoka kijiji cha Bejana katika kata ndogo ya Buni/Kisimani mjini Rabai, aliuawa na watu wasioijulikana saa kumi na moja alfajiri nje ya nyumba yake.

Mzee huyo alikuwa anajitawadha kwa maandalizi ya kuswali.

Kamanda wa Polisi wa Rabai, Bw Fredrick Abuga, alieleza kuwa kwa muda sasa polisi eneo hilo wamelivalia njuga suala la mauaji ya wazee ambalo limekuwa tata katika jamii za hapo.

“Visa vya mauaji ya wazee vimekithiri.Wengi wanaangamizwa kwa tuhuma za kuwa ni wachawi, sababu kuu ikiwa ni kutokana na mizozo ya mashamba,” akasema.

Hata hivyo, Bw Abuga alieleza kwamba eneobunge hilo la Rabai linaendelea kurekodi visa vichache vya mauaji ya wazee.

Hii ni kufuatia uhusiano mzuri wa wananchi na vyombo vya usalama.

Alidokeza kuwa mwaka huu ni visa vitatu tu vya mauaji aina hiyo vimeripotiwa.

Kulingana naye, katika mwaka wa 2019 takriban wazee watatu au wanne waliuawa kila wiki lakini kwa sasa juma linaisha bila kisa chochote.

Mwaka 2021, wazee wa Kaya wa Rabai waliitaka serikali kuunda jopokazi la kushughulikia mizozo ya mashamba katika eneo hilo ili kuzuia mauaji hayo.

Wakiongozwa na mwenyekiti Mzee Daniel Garero, walisema baadhi ya mauaji hutokana na madeni ya zamani yanayohusiana na ardhi, yaliyokuwepo kati ya mababu waliotangulia.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending