Connect with us

General News

Polisi wa akiba wamemwagwa Lamu, Elungata asema – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi wa akiba wamemwagwa Lamu, Elungata asema – Taifa Leo

Polisi wa akiba wamemwagwa Lamu, Elungata asema

NA KENYA NEWS AGENCY

KAMISHNA Mshirikishi wa Eneo la Pwani (RC) John Elungata amesema kwamba serikali imetuma polisi wa akiba wa kutosha katika Kaunti ya Lamu katika juhudi za kuimarisha usalama.

Bw Elungata amesema polisi hao wa akiba watawasaidia maafisa wa kulinda usalama eneo hilo na kuchukua hatua muhimu ya haraka kwa visa vya ukosefu wa usalama.

Alisema kutumwa kwa maafisa hao kutaimarisha usalama akieleza kuwa wanafahamu mandhari ya eneo hilo.

“Polisi wa akiba wanadhamiriwa kupiga jeki jukumu la maafisa wa kawaida wa polisi la kulinda usalama katika maeneo ya mashinani,” alisema.

Akizungumza Alhamisi katika Kituo cha Kibiashara cha Mokowe akiandamana na Bw Mbage Nganga, Kamishna wa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC), Bw Elungata alisema kuwa maafisa wa polisi wa akiba eneo hilo watasaidia kukabiliana na ukosefu wa usalama katika maeneo ya ndani ya Kisiwa cha Lamu.

Alisema maafisa hao watasaidia kukusanya habari mashinani na kushirikiana na mashirika ya usalama kurejesha amani na uthabiti kaunti hiyo.

Msimamizi mkuu huyo alisema polisi wa akiba watapokea msaada wanaohitaji kutoka kwa serikali ikiwemo ujira wa kuwasaidia kukimu mahitaji yao ya kimsingi.

Alisema kuwa maafisa wa akiba wanatarajiwa kuwa kikosi kikuu cha usalama katika vijiji hivyo kwa kuwa wanafanya kazi eneo lao.

Bw Elungata vilevile amewahakikishia walimu na wanafunzi kuhusu usalama wao wakati wa mitihani ya kitaifa kwa kuwa serikali imetuma maafisa wa kutosha eneo hilo.