Connect with us

General News

Polisi wachukue hatua na sio kupuuza maiti zilizopatikana Yala – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi wachukue hatua na sio kupuuza maiti zilizopatikana Yala – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Polisi wachukue hatua na sio kupuuza maiti zilizopatikana Yala

Na WANDERI KAMAU

KUMPOTEZA jamaa yako katika hali isiyoeleweka huenda ndilo jambo lenye uchungu zaidi katika maisha ya mwanadamu hapa duniani.

Ingawa kifo huwa na uchungu mkubwa, huwa kuna tulizo fulani jamaa wanapopata nafasi kuwaaga wapendwa wao waliowaondokea.

Hata hivyo, hali huwa kinyume jamaa yako anapopotea kwa miezi au hata miaka kadhaa, mnafanya juhudi kumtafuta hadi mnatamauka. Kabla ya kumsahau, mnaelezwa kuwa kuna miili iliyopatikana katika eneo fulani na kugundua kuwa yeye ni miongoni mwa miili iliyopatikana!

Taswira hiyo ya kuhofisha ndiyo imezikumba karibu familia 20, ambazo miili ya jamaa zao imepatikana imetupwa katika Mto Yala, Kaunti ya Siaya, kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Tayari, baadhi ya familia zimeitambua miili ya wapendwa wao waliopotea kwa miezi mingi bila kuelewa yaliyowakumba.

Haya yote yanapojiri, kinachosikitisha ni hali ya kutojali ambayo imedhihirishwa na Idara ya Polisi, kupitia msemaji wake, Bw Bruno Shioso.

Mara tu baada ya miili hiyo kupatikana, Bw Shioso alitoa taarifa akisema vyombo vya habari vinaupotosha umma kwa kusema kuwa miili ilipatikana kwa muda wa miezi mitatu badala ya miaka miwili.

Kwenye taarifa hiyo, Bw Shioso aliwarai Wakenya kutokubali “uwongo” uliokuwa ukienezwa na vyombo hivyo, akidai vingi havikuwa vimefanya utafiti wa kutosha.

Kimsingi, kile msemaji huyo anaonekana kusahau ni kuwa wanahabari huripoti matukio tofauti kulingana na maelezo wanayopata kutoka kwa wananchi.

Kamwe, hawawezi kujitengenezea taarifa kuhusu matukio watakayoandika au watayatangaza.

Vivyo hivyo, wenyeji wa eneo la Yala hawawezi kuidanganya nchi kuhusu matukio ambayo wamekuwa wakishuhudia karibu kila siku.

Ni wakati Bw Shioso akubali ukweli mchungu kuwa idara hiyo imezembea pakubwa kwenye jukumu lake la msingi la kutoa ulinzi kwa raia.

Ni sikitiko kubwa watu kutoweka na kutopatikana kwa hadi miezi mitatu katika nchi inayojivunia kuwa na idara ya polisi inayotumia teknolojia ya kisasa katika utendakazi wake.

[email protected]