[ad_1]
Polisi wahimizwa wakabili matapeli wanaohangaisha wananchi eneo la Mtwapa na Kilifi
Na ALEX KALAMA
IDARA ya polisi kaunti ya Kilifi imetakiwa kuingilia kati na kuwakamata matapeli wanaodaiwa kuwaibia wananchi kupitia mbinu zisizoeleweka katika kaunti hiyo.
Kulingana na afisa wa masuala ya dharura kutoka shirika la kutetea haki za kibinadamu la Muhuri Fransis Auma, wamepokea kesi takribani hamsini za watu ambao wamelalamikia kuibiwa pesa zao na matapeli hao.
Akizungumza na Taifa Leo mjini Kilifi, Bw Auma amevilaumu vitengo vya usalama katika kaunti hiyo pamoja na serikali ya kitaifa kwa kile anachodai kuwa, kutochukua hata licha ya waathiriwa kuripoti visa hivyo.
“Kumekuwa na visa vingi vya watu kulaghaiwa na kuibiwa pesa zao kupitia kwa simu hasa eneo la Mtwapa na Kilifi mjini lakini chakushangaza ni kwamba licha waathiriwa kuandikisha taarifa kwa polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya matapeli hao. Sasa tunajiuliza kazi ya polisi ni gani ikiwa tatizo kama hili wanashindwa kushughulikia,’’ alisema Bw Auma.
Afisa huyo amevitaka vitengo vya usalama kuwajibikia suala hilo na kuwaepusha watu na ulaghai huo.
“Tunataka polisi wafanye kazi waache kuzembea katika majukumu yao, kwa sababu kama tujuavyo kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia. Sasa ikiwa watawacha raia waendelee kuhangaishwa na watu wanaojifanya matapeli kazi yao itakuwa ni ipi,’’ alisema Bw Auma.
Ni kauli ambayo iliungwa mkono na Emmanuel Charo ambaye alitapeliwa na walaghai hao zaidi ya elfu kumi na tano wiki iliyopita.
Next article
Maafisa 30 kujiuzulu Nandi kugombea viti vya kisiasa 2022
[ad_2]
Source link