Connect with us

General News

Polisi wakubaliwa kuvunja makazi ya Mchina – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi wakubaliwa kuvunja makazi ya Mchina – Taifa Leo

Polisi wakubaliwa kuvunja makazi ya Mchina

NA RICHARD MUNGUTI

HAKIMU mwandamizi Philip Mutua amewaruhusu Polisi wavunje na waingie katika nyumba ya raia wa Uchina anayedaiwa alimchapa na kumuumiza mwenzake wanayeshtakiwa pamoja kwa ulaghai.

Bw Mutua alimruhusu Sajini Joram Karar kutoka kituo cha polisi cha Kilimani kuvunja makazi ya Zhu Jin Ping kumtia nguvuni.

Ping anaishi nyumba nambari 9 katika Planet Apartment.

Anatazamiwa kushtakiwa kumpiga na kumsababishia majeraha ya kudumu Li Xia aliyelazwa hospitalini kutokana na majeraha aliyopata.

“Ping alitekeleza makosa hayo miezi miwili iliyopita,” Sajini Karari alimweleza Bw Mutua.

Mahakama ilielezwa huenda Ping akatoroka humu nchini.

Bw Mutua alikubali ombi la Sajini Karari.