Connect with us

General News

Polisi wasaka walioharibu transfoma za SGR – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi wasaka walioharibu transfoma za SGR – Taifa Leo

Polisi wasaka walioharibu transfoma za SGR

Na PIUS MAUNDU

POLISI eneo la Ikoyo, Kaunti ya Makueni jana walianzisha msako wa watu wawili wanaodaiwa kuharibu transfoma inayotumika kutoa huduma kwa gari la moshi la SGR.

Wawili hao walishikwa kwenye kamera ya CCTV wakitenda uhalifu huo Jumamosi.“Wawili hao walitoroka na kuacha transfoma hiyo huku wakiwa na hofu ya kukamatwa. Tunatoa wito kwa umma ili wajitolee na kushirikiana na serikali kuwakamata wahalifu kama hao,” akasema Mohammed Maalim, kamanda wa polisi wa eneo hilo.

Haya yanajiri miezi michache baada ya wahalifu wengine kuharibu njia ya reli ya kisasa.Polisi hao wanasema kuwa kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu wanaoharibu vitu ambavyo vinafaa kuwanufaisha.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending