Connect with us

General News

Presha yamzidia Kalonzo aeleze msimamo upesi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Presha yamzidia Kalonzo aeleze msimamo upesi – Taifa Leo

Presha yamzidia Kalonzo aeleze msimamo upesi

NA BENSON MATHEKA

PRESHA inaongezeka kwa Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kufanya uamuzi kuhusu mwelekeo wake wa kisiasa huku uchaguzi mkuu wa Agosti 9 ukikaribia.

Washirika wake wa karibu, viongozi na wafuasi wanahisi kwamba makamu rais huyo wa zamani anawachelewesha ilhali wanataka kujua mwelekeo atakaochukua wajipange kama wa vyama na mirengo mingine ya kisiasa.

Bw Musyoka amekuwa akitoa ishara za kukanganya huku ikisemekana kwamba ananuia kuungana na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga katika vuguvugu la Azimio la Umoja.

Japo anasema kuwa nia ya muungano wa One Kenya Alliance (OKA) unaoshirikisha chama chake cha Wiper, Gideon Moi wa Kanu, Martha Karua wa Narc Kenya na Cyrus Jirongo wa United Democratic Party, utaungana na vyama na miungano iliyo na malengo sawa na yao, amekuwa akisema atakuwa kwenye debe.

Akiwa Kisii wiki jana, kabla ya kukutana na Bw Odinga mjini Mombasa Jumatatu wiki hii, Bw Musyoka alisema kwamba kujiunga kwa One Kenya Alliance katika Azimio la Umoja kutakuwa kupitia Rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, akiwa Kwale wiki hii alisema muungano huo hauna haraka ya kusuka ushirikiano wa miungano mingine.

Kauli hii ilitofautiana na aliyotoa Alhamisi alipojumuika na Bw Odinga na Bw Moi katika kongamano la kitaifa la wajumbe wa chama cha Jirongo alikoashiria kwamba OKA “inaimba wimbo mmoja na Azimio.”

Washirika wake wanahisi kwamba kutofanya uamuzi na kuchukua msimamo thabiti huku uchaguzi mkuu ukikaribia huenda kukawa pigo kwao hasa ikizingatiwa kwamba wapinzani wao katika viti mbali mbali wamechukua mwelekeo kwa kubaini sera, alama na rangi za vyama watakavyotumia.

Wadadisi wa siasa katika ngome yake ya Ukambani wanasema kujivuta kwa Bw Musyoka huenda kukaathiri umaarufu wake ikizingatiwa kwamba Naibu Rais Willam Ruto amepenya katika eneo hilo akisaidiwa na washirika wa zamani wa kiongozi huyo wa Wiper.

“Kupenya kwa Dkt Ruto eneo la Ukambani akisaidiwa na aliyekuwa seneta wa Machakos Johnstone Muthama na vita vya ubabe anavyopigwa na magavana watatu wa kaunti za eneo hilo kunaweza kufifisha umaarufu wake na wa chama cha Wiper,” alisema John Kisilu, mchanganuzi wa siasa.

Magavana Alfred Mutua (Machakos) Charity Ngilu (Kitui) na Kivutha Kibwana (Makueni) wamekuwa wakimtaka Bw Musyoka kuungana na Bw Odinga katika Azimio la Umoja.

Duru zinasema Bw Musyoka amekuwa akifanya mazungumzo na Bw Odinga kupitia wandani wao wasio wanasiasa.

Hii imeacha gizani washirika wake wa kisiasa wakiwemo wabunge, maseneta na maafisa wa chama chake.

“Hii ndiyo inafanya wabunge wanaomuunga mkono kumshinikiza kuweka wazi hatua alizofikia kwa kuwa chama kilimpa idhini ya kujadiliana na vinara na vyama vya kisiasa kwa nia ya kuunda muungano wa kisiasa. Lakini sasa wanahisi kwamba anawachelewesha,” asema Susan Kasila, msomi na mchanganuzi wa siasa za Ukambani.

Anasema kwamba kuwaacha washirika wake gizani kumesababisha kiwewe huku ikiibuka kuwa kulingana na mkataba wa OKA, vyama tanzu vinapaswa kufanya uamuzi wa pamoja.

Mmoja wa wandani wa Kalonzo ambaye aliomba tusitaje jina alisema Bw Musyoka anatumia OKA na hataki kuonekana kusaliti vinara wenza kwa kuamua kuingiza Wiper katika Azimio.

“Mipango imekamilika (ya kuunga Azimio) lakini kupitia OKA. Ni mchakato unaokita katika msingi wa sheria mpya ya miungano na kwa hivyo, mambo yakiiva, kila mmoja atajua,” akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending