Connect with us

General News

Raia wataka suluhisho kuhusu umiliki wa fuo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raia wataka suluhisho kuhusu umiliki wa fuo – Taifa Leo

Raia wataka suluhisho kuhusu umiliki wa fuo

NA MAUREEN ONGALA

UJENZI wa nyumba za kifahari katika fuo za bahari Kaunti ya Kilifi, umeanza kuibua malalamishi miongoni mwa baadhi ya wakazi.

Huku wenye nyumba hizo wakitaka kujihakikishiwa usalama wao, hatua ambazo wamekuwa wakichukua, kama vile kufanya fuo wanazopakana nazo kuwa za kibinafsi, zimesababisha umma kuzuiwa kutumia fuo hizo ambazo awali zilikuwa wazi kwa wananchi.

Katika kisa cha hivi majuzi, vijana katika kaunti hiyo waliamkia hasara tele walipopata vibanda ambavyo walikuwa wakitumia kibiashara ufuoni vimebomolewa.

Wamelalamikia kukatazwa kutumia ufuo wa bahari kujiendeleza na kupata pato la kila siku. Sasa wametoa wito kwa viongozi wa kaunti na serikali ya kitaifa kuingilia kati ili kutatua mizozo kati yao na wawekezaji wanaodaiwa wamenunua ardhi zinazopakana na sehemu hizo za ufuo.

Huwa inadaiwa kuwa, vijana hao huchafua mazingira kwa takataka na kelele wanapoendeleza biashara zao.

Jumamosi iliyopita, watu wasiojulikana walibomoa hoteli na sehemu za kustarehe zinazomilikiwa na kundi la vijana la B-10 Self Help Group katika ufuo wa B-10 katika ufuo wa bahari wa Bora.

Katika kisa hicho kilichotokea usiku, walipoteza mali ya takriban Sh3.5 millioni.

Vijana katika ufuo wa bahari wa Vidadzini pia walivunjiwa vibanda vyao vya biashara siku hiyo.

Mwanzilishi wa kundi la B-10 Self – Help Goup, Bw Douglas Mujidu, alisema inasikitisha kuwa wanaendelea kupata vikwazo wakati serikali inaposema inajitahidi kuimarisha uchumi wa sekta ya baharini.

“Kila mara tunasikia kuwa serikali inaendeleza juhudi za kuimarisha uchumi wa bahari lakini tunashangaa mpango huo utafaulu vipi ikiwa vijana wanakatazwa kufaidika na bahari,” akasema.

Alieleza kuwa biashara hiyo iliyosambaratishwa ilianzishwa mwaka wa 2019 na vijana kutoka kwa akiba yao. Walikuwa wakiuza bidhaa tofauti kwa minajili ya kupata pato la kila siku na pia kutoa nafasi za kazi kwa wenzao.

Bw Mujibu alisema kuwa walilenga kupanua biashara hiyo ili kutoa nafasi za ajira nyingi kwa jamii.

Mbali na watalii wa humu nchini, watalii kutoka nchi za ng’ambo pia walikuwa wakizuru ufuo huo kujifurahisha.

“Kusambaratishwa kwa biashara hii si pigo kwa vijana tu bali kwa jamii nzima waliokuwa wanategemea kupata pesa za kujikimu,” akasema.

Kulingana na Bw Mujibu, maafisa wa polisi walikuwa katika maeneo hayo kutoa ulinzi wakati tingatinga lilipokuwa linabomoa.

Hata hivyo, Kamanda wa polisi wa eneobunge la Kilifi Kaskazini, Bw Jonathan Koech, alikana madai kuwa polisi walihusika na ubomozi huo.

“Tulipigiwa simu na vijana hao na OCS wa kituo cha polisi cha Kilifi al – ifika maeneo hayo na kuthibitisha tukio hilo, lakini hatukupata mshukiwa yeyote,” akasema.

Alisema hawajaweza kubainisha iwapo polisi walikuwa katika maeneo hayo walikuwa wa kutoka wapi.

Mfanyabiashara mwingine, Bw Sadiki Ote, alisema kuanzisha kwa biashara katika ufuo huo wa bahari ulikuwa umezuia uhalifu.

Alisema kwamba hapo awali mwaka wa 2018 na nyuma ufuo huo ulitumika kama maficho ya wahali – fu.

Bishara haramu ya dawa za kulevya, dhuluma dhidi ya jinsia kwa vijana na wasichana wadogo na wizi ni baadhi ya uhalifu uliokuwa unatekelezwa huko.

Zaidi ya vijana 30 walikuwa wameajiriwa kama wapishi, wahudumu na walinzi miongoni mwa watoaji wa huduma nyinginezo.