Connect with us

General News

Raila aidhinisha Fernandes Barasa awe mrithi wa Oparanya Kakamega – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raila aidhinisha Fernandes Barasa awe mrithi wa Oparanya Kakamega – Taifa Leo

Raila aidhinisha Fernandes Barasa awe mrithi wa Oparanya Kakamega

NA CHARLES WASONGA

NI bayana kuwa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) hakitaandaa mchujo wa ugavana katika kaunti ya Kakamega.

Hii ni baada ya kiongozi wa chama hicho Raila Odinga Jumamosi, Machi 26, 2022 kumwidhinisha aliyeku mkurugenzi mkuu wa kampuni ya umeme, Ketraco, Fernandes Barasa kuwa mgombeaji wa kiti hicho kwa tiketi ya chama hicho cha Chungwa.

“Tuko na Barasa hapa ambaye ni kijana yangu. Yeye ndiye sasa atachukua nafasi ya Oparanya ya ugavana wa Kakamega. Si anatosha?” Bw Odinga akauliza umati alipokuwa akifanya kampeni katika kituo cha kibiashara cha Sabatia, eneobunge la Butere, kaunti ya Kakamega.

Hatua hiyo inaashiria kuwa Bw Barasa ndiye atapeperusha bendera ya ODM katika kinyang’anyiro cha ugavana wa Kakamega Agosti.

Hii ina maana kuwa chama hicho hakitaandaa mchujo wa kuteua mgombeaji wake katika kiti hicho, zoezi ambalo liliratibiwa kuanza mwezi ujao wa Aprili.

Bw Barasa sasa atakabiliana debeni na Seneta wa Kakamega Cleophas Malala (ANC) ambaye juzi aliidhinishwa na Naibu Rais William Ruto kupeperusha bendera ya muungano wa Kenya Kwanza.

Uidhinishwaji wa Bw Malala ulijiri baada ya vinara wa muungano huo wakiongozwa na Dkt Ruto kufaulu kumpatanisha na seneta wa zamani Boni Khalwale ambaye alitaka kuwania kiti hicho cha tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Dkt Khalwale sasa atakuwa mwaniaji useneta wa Kakamega chini ya udhamini wa Kenya Kwanza.

Bw Malala na Dkt Khalwale wamekuwa wakivutania kiti hicho kwa muda sasa kila mmoja akidai ndiye anafaa kupeperusha bendera ya Kenya Kwanza katika kinyang’anyiro cha ugavana.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending