Connect with us

General News

Raila amteua Makau Mutua kuongoza kampeni zake za urais – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raila amteua Makau Mutua kuongoza kampeni zake za urais – Taifa Leo

Raila amteua Makau Mutua kuongoza kampeni zake za urais

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga amemteua mwanasheria mashuhuri Profesa Makau Mutua kuwa msemaji na mwanachama wa jopo la kupanga mikakati ya kampeni zake za urais.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Jumanne, Bw Odinga alisema jopo hilo linatarajiwa kutoa mwongozo wa kisera kwa bodi ya kushirikisha kampeni zake za urais inayoongozwa na Gavana wa Laikipia Ndiritu Muriithi.

‘Nina matumaini kuwa ushauri wako wa busara utaniwezesha kufaulu katika safari hii. Inawezekana” Bw Odinga akasema.

Prof Mutua ambaye ni mhadhiri wa zamani wa Kitivo cha Sheria cha Buffalo, Chuo Kikuu cha New York, atahudumu kama msemaji rasmi wa kampeni za urais za Bw Odinga.

Profesa Mutua pia ni mwandishi wa makala katika Gazeti la Sunday Nation, amekuwa mfuasi sugu wa Bw Odinga tangu 2007.

Baada ya uteuzi wake, msomi huyo alituma ujumbe kupitia Twitter akimpongeza Bw Odinga kwa kumtunuku wadhifa huo wenye “hadhi ya kipekee.”

Aliongeza kuwa amejitolea kumhakikisha kuwa kiongozi huyo wa ODM anashinda uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

“Asante Bw Raila kwa kuniamini na kunipa hadhi hii ya kipekee na kukutumikia na watu wa Kenya katika nafasi hizi muhimu. Naamini tutafaulu katika mipango yetu ya kuhakikisha unaingia Ikulu,” Prof Mutua akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending