Connect with us

General News

Raila kumlemea Ruto debeni sasa – Utafiti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raila kumlemea Ruto debeni sasa – Utafiti – Taifa Leo

Raila kumlemea Ruto debeni sasa – Utafiti

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Rais William Ruto, ana kibarua kigumu kumpiku Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga kwa umaarufu katika Kaunti ya Mombasa kabla uchaguzi ujao wa urais kwa mujibu wa matokeo ya utafiti.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la utafiti la Infotrak, umebainisha kuwa, ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Gavana wa Mombasa, Bw Hassan Joho, huenda ukamlemea sana Dkt Ruto katika eneo hilo.

Matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa Jumapili yalibainisha kuwa, endapo Uchaguzi Mkuu ungefanywa leo, Bw Odinga angezoa asilimia 52 za kura Mombasa huku Dkt Ruto akipata asilimia 29 pekee.

Kaunti ya Mombasa ndiyo huongoza kwa idadi ya wapigakura baina ya kaunti zote sita za Pwani na pia huaminika kutoa mwelekeo wa siasa za kitaifa katika ukanda huo.

Takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) zaonyesha kuwa, katika mwaka wa 2017, kaunti hiyo ilikuwa na wapigakura 580,644.

Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.Utafiti wa Infotrak pia umeonyesha kuwa, Bw Musyoka ambaye anaegemea upande wa Bw Odinga, angepata asilimia moja tu za kura za urais, naye Kiongozi wa Chama cha Amani National Congress (ANC), Bw Musalia Mudavadi, aliye upande wa Dkt Ruto, angepokea asilimia 0.1 za kura za urais Mombasa.

Hata hivyo, kuna asilimia 16 ya wapigakura ambao bado wanaweza kung’ang’aniwa na wanasiasa wanaomezea mate urais kwani idadi hiyo haijaamua yule wanayemtaka.

Kulingana na utafiti huo, Bw Odinga ana umaarufu wa zaidi ya asilimia 50 katika maeneobunge manne kati ya sita yaliyo Mombasa.

Maeneo ambapo umaarufu wake uko juu zaidi ni Jomvu (asilimia 56), Kisauni (asilimia 54), Likoni (asilimia 53) na Changamwe (asilimia 51).

Hata hivyo, inaonekana atahitajika kutia bidii katika eneobunge la Nyali na Mvita ambapo umaarufu wake ni asilimia 49.

Maeneobunge hayo mawili ndipo umaarufu wa Dkt Ruto uko juu kuliko katika maeneobunge mengine, kwani ana asilimia 35 Nyali na asilimia 33 Mvita.

Umaarufu wake eneobunge la Changamwe ni asilimia 30, Likoni asilimia 29, Kisauni asilimia 23 na Jomvu asilimia 26.

Kampeni za Dkt Ruto katika eneobunge la Nyali zimekuwa zikiandaliwa kwa ushirikiano na Mbunge wa eneo hilo, Bw Mohamed Ali, ambaye alishinda kiti hicho kama mgombea huru 2017.

Haikubainika wazi sababu za Bw Odinga kuteleza Mvita.

Kando na hayo, ripoti ya utafiti huo uliofadhiliwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Africa imeonyesha kwamba, Chama cha ODM kimedhibiti Mombasa kwa umaarufu.

Umaarufu wa ODM kaunti hiyo ni asilimia 46 huku kile cha United Democratic Alliance (UDA) ukiwa asilimia 24.Vile vile, umaarufu wa Muungano wa Azimio la Umoja ni asilimia 51 huku Kenya Kwanza ukiwa asilimia 23.

Mabw Odinga, Kenyatta na Joho wanaongoza kwa ushawishi wa kisiasa kaunti hiyo kwa asilimia 59, 54 na 53 mtawalia, huku ushawishi wa Dkt Ruto ukiwa ni asilimia 48.

Ushawishi wa Bw Musyoka katika kaunti hiyo ni asilimia 32.

Makundi mengine yaliyo na ushawishi wa kisiasa katika kaunti hiyo ni wafanyabiashara (asilimia 42) na wazee wa Kaya za Mijikenda (asilimia 39).

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending