Kila siku ya wiki, TUKO.co.ke inakupakulia kwa mukhtasari matukio na habari muhimu zilizogonga vichwa vya habari wiki hii ili ukapate kufahamu kwa upana na utendeti mambo yalivyo ulimwenguni.
Daktari wa kwanza nchini Kenya aliyefariki duniani kutokana na ugonjwa hatari wa corona amezikwa nyumbani kwake kaunti ya Bungoma hii leo Jumatatu, Julai 13.
Hafla yake ya mazishi ilihudhuriwa na waombolezaji wachache ikiwa ni moja wapo wa masharti yaliowekwa na wizara ya afya ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya COVID- 19.
Daktari Lugaliki alifariki dunia kutokana na ugonjwa hatari wa corona aktari Doreen Lugaliki. Source: UGC
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alirejea nchini kimya kimya majuma matatu baada ya kulazwa katika hospitali moja kule Dubai ambapo amekuwa akipokea matibabu.
Raila alitua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta Jumapili, Julai 12. Source: Facebook
Zindzi ambaye alifariki mjini Johannesburg mapema Jumatatu, Julai 13 akiwa na miaka 59, alihusika katika vita vya kupigania uhuru nchini Afrika Kusini.
Mama huyo msimbe ambaye aliondoka kwa uhusiano huo baada ya kuzuka kwa kashfa ya KSh 310, alifichua kwamba alianza kuishi pamoja na mtumishi huyo wa Mungu wiki tatu baada ya wao kuchumbiana.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.