Connect with us

General News

Rais Kenyatta asema serikali yake imeboresha sekta ya ICT – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Rais Kenyatta asema serikali yake imeboresha sekta ya ICT – Taifa Leo

Rais Kenyatta asema serikali yake imeboresha sekta ya ICT

NA SAMMY WAWERU

MADARAKA Dei 2022 ilikuwa hafla ya mwisho ya kitaifa kwa Rais Uhuru Kenyatta akikamilisha kipindi chake cha uongozi.

Akiwa rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya, amehudumu mihula miwili kati ya 2013 – 2022, akisaidiwa na naibu wake, William Ruto.

Wawili hao licha ya kuwa kwa sasa wanatofautiana kisiasa, walichaguliwa kama rais na naibu, mtawalia.

Katika maadhimisho ya Makala ya 59 ya sherehe za Madaraka, yaliyofanyika Jumatano Uhuru Gardens, jijini Nairobi, Rais Kenyatta alisifia serikali yake ya Jubilee katika kuboresha sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia (ICT).

Kiongozi wa nchi alisema ni chini ya utawala wake, vituo vya runinga viliongezeka kutoka 14 mwaka 2013 hadi 130, na redio 204, juu kutoka vituo 130, kupitia uhamaji wa analogi kuingia mfumo wa kidijitali.

“Ni hatua ambayo imesaidia kubuni nafasi tele za ajira,” Rais akasema.

Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta alisema ni kutokana na ukuaji wa ICT, matumizi ya intaneti yameboreka kutoka asilimia 31.4 mwaka 2013 hadi asilimia 93.9 mwaka huu, 2022.

Bw Joe Mucheru ndiye Waziri wa ICT.

“Isitoshe, matumizi ya simu za rununu yamekua kutoka asilimia 74.9 mwaka 2013 hadi asilimia 131 mwaka huu. Usambazaji wa pesa kwa njia ya simu tamba, umeongezeka kutoka Sh1.9 trilioni hadi Sh6.8 trilioni,” Rais Kenyatta akaelezea.

Alisema mipango ya serikali kubuni nafasi za ajira kwa njia ya mitandao, imechangia kuwepo kwa nafasi za kazi karibu milioni moja, ubunifu wa wananchi ukiiweka Kenya katika ramani ya ulimwengu.

Kupitia mpango wa Ajira Digital, baadhi ya vijana wanaendelea kunufaika kwa mianya mbalimbali ya kazi.

Rais Kenyatta alisisitiza kwamba atafurahia kupata mrithi atakayeendeleza mipango na miradi ya maendeleo aliyoanzisha.

Aidha, kiongozi wa nchi ameweka wazi kwamba anaunga mkono kinara wa Azimio, Raila Odinga kumrithi.

Katika uchaguzi mkuu mwaka huu, Bw Odinga (ODM) ambaye amewahi kuhudumu kama Waziri Mkuu chini ya utawala wa Rais (mstaafu) Mwai Kibaki, ambaye ni marehemu, atapeperusha bendera ya urais akisaidiwa na mgombea mwenza Bi Martha Karua (Narc-Kenya).

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending