Connect with us

General News

Refa Lucy Wanjiru aamini kufaulu kunatokana na mtu kupenda kazi yake – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Refa Lucy Wanjiru aamini kufaulu kunatokana na mtu kupenda kazi yake – Taifa Leo

Refa Lucy Wanjiru aamini kufaulu kunatokana na mtu kupenda kazi yake

NA PATRICK KILAVUKA

KUWA na matumaini katika ulitakalo huwa chimbuko la mawazo ya kujiwazia mema na hamu ya kufaulu katika hali yoyote ile ya mwanadamu!

Hiyo ni kauli ya refa Lucy Wanjiru, 24 ambaye hata hivyo anasema safari yake ya kuwa refa haikuwa rahisi.

Refa huyu ambaye ni mzaliwa wa Njoro, Kaunti ya Nakuru alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Ngongogeri kabla kujiunga na sekondari ya Ogilgei.

Anasema alianza kama mchezaji. Alikuwa difenda akiwa shule ya msingi na huko alipiga soka hadi kiwango cha Kaunti ya Nakuru na akiwa shule ya upili alikumbatia kabumbu hadi Kiwango cha Kanda ya Kusini mwa Bonde la Ufa.

Ni baada ya kumaliza masomo ya upili ambapo alipata fursa ya kujitanua katika fani ya soka kwa kujiunga na timu ya Kibagare Girls mwaka 2017 na kujituma 2019 na wakatwaa taji la Tim Wanyonyi Super kwa kushinda Kangemi Ladies 2-0 ugani CAVS.

Baada ya msambao wa corona kuyeyuka kiasi na milango ya soka kufunguliwa, muamuzi huyu alianza kusakamwa na kiu ya kuendeleza taaluma yake katika ulingo wa kandanda na kuona kwamba njia ya pekee anaweza kufuatilia ndoto yake ni kuwa mpuliza kipenga mbali na kufanya kazi ya kudumisha usafi wa majumba kupitia kampuni ya Arrow Facilities.

Alishawishiwa na kinara wa marefa tawi la Nairobi Magharibi Aggrey Shavera kupata fursa ya kujifunza kozi ya urefa kwa wiki moja na kupita mtihani wa kiwango cha gredi ya tatu.

Baada ya mafunzo, alianza kuchezesha mechi za Shirikisho la Kandanda kaunti ndogo, Kaunti na Kanda mwaka 2021.

Mechi ya kwanza kuchezesha ilikuwa Uthiru Vision dhidi ya Kangemi PAG kama refa msaidizi kabla kuaminiwa uchezeshaji wa kati.

Amechezesha mwaka huu kinyang’anyiro cha Westlands Youth Soccer Tournment almaarufu kama Tim Wanyonyi Super Cup kitengo cha shule za upili.

Alichezesha kwa busara kubwa pia mchuano wa Ligi ya Kaunti ndogo ya Kabete baina ya White Eagles dhidi ya Kabete Pirates na kuridhisha mashabiki na wadau wa timu hizo pasi na kuteleza katika wajibu wake urefa.

Ari ya kufikia upeo wa taaluma yake ya urefa, imetokana na refa ambaye ni kielelezo chake refa wa Fifa Bruce Philiph na mwenyekiti wa marefa Shavera.

“Mawaidha ya wazoefu hao niliowataja kama kivutio changu, yamenifanikisha katika uwanja huu kwani yamenipanua kimawazo na kimaamuzi na wananihimiza kuzingatia kanuni za soka kujipiga jeki katika utekelezaji wa majukumu ya mpuliza firimbi,” anasema refa Lucy ambaye amebarikiwa mtoto Blessing Wairimu.

Yeye hujinoa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa baada ya kazi kabla kuwajibishwa wikendi.

Refa Lucy Wanjiru (kushoto) akiwa katikati mwa uwanja kuchezesha mchuano wa White Eagles (jezi nyekundu) dhidi ya Kabete Pirates uwanjani Approved, Lower Kabete. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Anasema kujihakikishia kwamba anakita mizizi, hujijasirika akiwa ugani, kuwa radhi kuendelea kusoma sheria za kandanda, kufanya mazoezi kwa bidii na kujinyanyua zaidi.

Changamoto ambaye amekumbana nazo ni mizomeo ya mashabiki ambao wanataka timu zao zishinde pasi na suala la kitaasubi.

Anajipiga moyo konde kuwa refa wa Fifa usoni.

Ushauri wake ni kwamba ukitakuwa refa,fuata ndoto yako na penda ikifanyacho.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending