Connect with us

General News

Ringtone ana wivu, acha tu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ringtone ana wivu, acha tu – Taifa Leo

DOMO: Ringtone ana wivu, acha tu

NA MWANAMIPASHO

WAJUA kuna watu wenye tabia chwara wafananao na majina yao. Kwa mfano huyu msanii wa injili aitwaye Alex Apoko au ukipenda Ringtone.

Nadiriki kusema hapa kuwa Ringtone ni moja kati ya wasanii wa ajabu kuwahi kutokea katika taifa hili.

Unapokuwa na mtu ambaye kazi yako kila kukicha ni kukashifu maendeleo ya wasanii wenzako, basi una kasoro.

Ringtone ana ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, umaarufu aliojijengea kwa unyenyekevu kama unakumbuka zile enzi za Pamela.

Ila ameondokea kuwa mtu anayekwaza sio tu mashabiki bali pia wasanii wenzake.

Kila leo, jamaa lazima aibuke na ishu ya ovyo sijui kwa kutaka kutrendi au kwa faida gani.

Kila leo lazima atapinga jambo jema la msanii mwenzake.

Juzi nimemwona akimwingilia Nyashinski baada ya jamaa kujaza ukumbi wa Carnivore kwa shoo yake mwenyewe Shin City.

Ilivyo ada yake, Ringtone alitaka kusikika hivyo akatumia njia yake ya bora ya kujishaua, Instagram.

Pale alidhihaki shoo ya Nyashinski ambayo ilikuwa yeye mafanikio makubwa. Ni dhahiri wivu ulimzidia Ringtone ukizingatia kuwa alimsuta Nyashinski kwa kauli ya kipuzi akidai kuwa jamaa alikesha kuwatumbuiza walevi.

Sijawahi kumchukulia Ringtone na akili zake za kitoto kwa uzito. Huwa muda wote ni mwingi wa maneno ila mchache wa hoja.

Kumkashifu Nyashinski ni sawa kama dhamira yake ilihisi alichofanya sio sawa. Lakini hakustahili kutuonyesha uzuzu wake kwa kujaribu kuchafua picha safi.

Niliposoma kauli yake, nilikaa na kuwaza, hivi huyu Ringtone ana mchango upi wa maana kwenye tasnia ya sasa ya burudani? Hakuna.

Zaidi ya umbea wa kipuzi Instagramu, sioni la maana analofaidi gemu. Mara ya mwisho yeye kutoa hiti nilikuwa bado sijaota kitambi.

Nilikuwa bado nimeparara nahangaika kusaka maisha. Mtu kama Nyash aliyeacha gemu, karudi na kuiteka himaya yake, himaya ambayo Apoko hawezani nayo.

Ikiwa Apoko anahisi Nyashinski alichokifanya ni jambo ndogo, mbona yeye asituandalie shoo yake ya kipekee, ili tushuhudie uwezo wake wa kuwazengua mashabiki.Hivi ni nani atakwenda kwenye shoo ya jamaa nauliza.

Nina uhakika hata jamaa na familia yake watashindwa kuhudhuria. Hata itokee shoo nyenyewe kiingilio ni bure, Apoko atajikuta akijitumbuzia mwenyewe.

Ukweli ni kuwa muziki ulimshinda jamaa na inamuuma kuona wenzake waliofanikiwa kupata ujanja wa kuziboresha brandi zao. Ndio sababu alipoalikwa kwenye uzinduzi wa albamu ya Size 8 nusura alimwe mangumi na DJ Mo kwa sababu ya mawazo yake mafupi.

Wakati mwingine sio lazima utolee jambo hoja kama huna la kusema. Sio kila jambo linahitaji mtazamo. Sijui anafaidi nini kwa tabia hii sababu ameishi kuwa nayo. Au pengine anafurahiaga kuwakera watu. Unaweza kuona ni kwa nini mwaka jana bloga Robert Alai aliamua kumtoa jamaa manundu kwa kumlima na rungu la kimasaai. Huyu jamaa ni kero tosha. Ana PhD ya kusinya huyu!

Kheri kero za usumbufu wa mbu, kuliko Apoko.