[ad_1]
Ruto akausha mahasla kwa kukosa kuwasili kuwachangishia pesa
Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais William Ruto aliwaacha wafuasi wake na njaa alipokosa kuhudhuria hafla ya kuchangisha pesa makanisa 35 katika Kaunti ya Nyamira, jambo ambalo liliwakasirisha waliokuwa wakimsubiri.
Dkt Ruto alitarajiwa kuzuru eneobunge la Mugirango Magharibi kwa harambee ya makanisa, na kukutana na mahasla waliotarajia angewaachia pesa za kujiinua anavyofanya anakozuru.Harambee hiyo ingefaidi zaidi ya makanisa 35 lakini hilo halikufanyika baada ya wandani wa Dkt Ruto kueleza waumini kuwa hangefika.
Siku hiyo Naibu Rais alikuwa akizuru Kaunti ya Nyeri.Ilibidi mbunge wa eneo hilo Vincent Kemosi aingilie kati na kuomba radhi kwa niaba ya Dkt Ruto baada ya waumini hao kuchoka kumngoja.“Mnajua Naibu Rais ana shughuli nyingi.
Wakati wote amekuwa akisema atafika hapa lakini safari zake za kukutana na Wakenya zimekuwa nyingi, lakini ameahidi atapanga kuja baadaye,” Bw Kemosi akasema.Bw Kemosi aliandamana na mbunge wa Borabu Ben Momanyi katika hafla hiyo ya Jumapili katika kanisa katoliki la Nyansabakwa na Omosasa Lutheran, Bobembe.
Bw Momanyi kwa siku nyingi ameonekana kumshabikia Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake katika handisheki, Raila Odinga.Licha ya kutozungumzia sana siasa za kitaifa, mbunge huyo wa Borabu anayelenga kuwania kiti cha ugavana Nyamira mwaka ujao, aliamua kutumia fursa hiyo kujipigia debe na kuomba wakazi wa Nyamira wamuunge mkono awe gavana wao wa tatu.
Next article
Juventus wakomoa Genoa na kupaa hadi nafasi ya tano Serie A
[ad_2]
Source link