Connect with us

General News

Ruto ana kibarua kudumisha ubabe wake Mlima Kenya baada ya mchujo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ruto ana kibarua kudumisha ubabe wake Mlima Kenya baada ya mchujo – Taifa Leo

CECIL ODONGO: Ruto ana kibarua kudumisha ubabe wake Mlima Kenya baada ya mchujo

NA CECIL ODONGO

NAIBU Rais Dkt William Ruto atakuwa na kibarua kigumu kudumisha ubabe wa UDA eneo la Kati baada ya mchujo wa wiki jana kuwagawanya mno wafuasi wa chama hicho Mlima Kenya.

Eneo la Mlima Kenya limekuwa likionekana kuwa ngome ya Dkt Ruto kutokana na idadi kubwa ya viongozi ambao wamekuwa wakimuunga mkono ikikisiwa hili lilitokana na kumpigia debe Rais Uhuru Kenyatta katika chaguzi za 2013 na 2017.

Hata hivyo, mgawanyiko huo sasa umesababisha baadhi ya wanasiasa ambao wanahisi mchujo huo ulivurugwa kutishia kuhama UDA na kuwania viti wanavyovilenga kama wawaniaji huru kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Kwanza, kumekuwa na madai kuwa baadhi ya wanasiasa maarufu waliobwagwa kwenye mchujo huo, walilemewa kutokana na njama ya uongozi wa chama kwa sababu wao ni tishio kwa umaarufu wa Dkt Ruto katika kudhibiti eneo hilo kisiasa siku zijazo.

Inadaiwa mbinu hii ndiyo ilitumika na Dkt Ruto kuelekea uchaguzi wa 2017 ambapo baadhi ya wanasiasa waliokuwa washirika wa karibu wa Rais Uhuru Kenyatta waliangushwa kwenye mchujo wa Jubilee.

Mara hii kumekuwa na malalamishi kwa kuwa wengi wa wanasiasa wanaohudumu sasa hasa katika eneo hilo waliwika katika mchujo kwa sababu Dkt Ruto angependelea kuendeleza kujenga himaya yake ya kisiasa eneo hilo akiwatumia baadhi yao.

Hata hivyo, hii itakuwa hatari kwa Naibu Rais kwa sababu iwapo wanasiasa hawa wataangushwa debeni na wenzao waliopoteza mchujoni kisha kugombea kama wawaniaji huru, ushawishi wake wa kisiasa katika eneo hilo utadidimia zaidi hasa akipoteza Urais.

Vilevile, idadi ya waliojitokeza katika kura ya mchujo Mlima Kenya ilikuwa ya chini ikilinganishwa na wale katika ngome ya Dkt Ruto ya Bonde la Ufa licha ya uteuzi huo kuendeshwa na sajili ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC).

Hii ni kinyume na hadhara mkubwa ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika mikutano ya Dkt Ruto katika eneo hilo. Kujitokeza huko kunafaa kumtia wasiwasi Dkt Ruto kuwa huenda wengi hawatajitokeza kumpigia kura jinsi ilivyokuwa kwa Rais Kenyatta katika chaguzi za 2013 na 2017 hasa wakati huu hawana mwaniaji maarufu anayelenga uongozi wa nchi.

Kando na hayo, Rais Kenyatta tayari ametangaza kuwa analenga kuimarisha kampeni za mwaniaji wa Urais wa muungano wa Azimio-One Kenya, Raila Odinga mwezi ujao katika kaunti za Mlima Kenya baada ya IEBC kutangaza rasmi kuwa muda wa kampeni uanze.

Iwapo waasi wa UDA wataungana na wale wa Azimio na kumvumisha Bw Odinga, basi ni Naibu Rais atapoteza zaidi kwa sababu sehemu za kura alizokuwa akilenga zitamwendea waziri huyo mkuu wa zamani.

Jinsi hali ilivyo kwa sasa, Dkt Ruto atajihakikishia kura za Mlima Kenya iwapo atamteua mwaniaji mwenza kutoka ukanda huo licha ya raia kuwa nafasi hiyo iendee Musalia Mudavadi wa ANC.

Akikosa kutoa nafasi hiyo kwa eneo la Mlima Kenya, basi huenda uungwaji mkono wake ukapungua hasa kama Azimio la Umoja-One Kenya Alliance itamteua mwaniaji mwenza wa Bw Odinga kutoka eneo hilo.

Kutokana na mpasuko ulioshuhudiwa katika mchujo wa UDA na mkondo wa siasa nchini, Dkt Ruto lazima acheze karata yake vyema ili kudumisha uungwaji mkono Mlima Kenya na kuhakikisha wengi wanajitokeza siku ya uchaguzi kumpigia kura.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending