Connect with us

General News

Sababu za Kiswahili kupendelewa dhidi ya lugha za asili nchini Kenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sababu za Kiswahili kupendelewa dhidi ya lugha za asili nchini Kenya – Taifa Leo

NGUVU ZA HOJA: Sababu za Kiswahili kupendelewa dhidi ya lugha za asili nchini Kenya

NA PROF IRIBE MWANGI

JUMA hili tunasherehekea lugha za KiAfrika.

Kama nilivyoeleza majuma mawili yaliyopita, Kiswahili ni mojawapo ya lugha hizo za KiAfrika yenye unasaba wa KiBantu.

Kwa hakika, Kiswahili ni lugha asili ya Afrika yenye wazungumzaji wanaoitumia kama lugha ya kwanza wapatao milioni 15 kote Afrika. Nchini Kenya, wazungumzaji wake ni zaidi ya 130,000.

Hata hivyo, idadi hii ni ndogo sana (asilimia 0.32) ikilinganishwa na wazawa wa lugha nyinginezo.

Bighairi ya hilo, Kiswahili kimependelewa na kupewa hadhi maalum nchini kwa kuteuliwa kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi.

Je, kwa nini kikapendelewa hivi?

Kuna sababu nyingi. Sababu ya kwanza ni huo uchache wa wazungumzaji asili.

Suala la upangaji lugha ni la kisiasa.

Kwa sababu hiyo, kisiasa, inaonekana mwafaka kusambaza lugha yenye watumizi wachache kuliko ile yenye wazawa wengi ambayo uchukulio wake huweza kuwa hasi.

Sababu nyingine ni kuwa, kama tulivyoonyesha juma lililopita, Kiswahili kimeenea sana na kwa sababu hiyo kimepata watu wengi wanaokitumia kama lugha ya pili.

Pia, Waswahili ndio waliokuwa wa kwanza kukutana na wageni walipofika pwani.

Kutokana na hilo, Kiswahili kilianza kutumiwa katika maandishi (kwa hati za KiArabu na KiRumi) kitambo ikilinganishwa na lugha nyinginezo za Kenya.

Kwa hakika, ndiyo iliyokuwa lugha ya kwanza kusanifishwa. Zaidi ya haya yote, kulikuwa na msukumo mkubwa wa wananchi kwa Serikali kukipa Kiswahili hadhi maalum.

Asilimia 62 ya lugha za Kenya zina asili ya KiBantu kama kilivyo Kiswahili.

Kwa sababu hiyo, kutokana na kufanana kwa miundo, inakuwa rahisi kwa Wakenya wengi kujifunza Kiswahili.