Connect with us

General News

Safaricom yafunga duka lake baada ya wafanyakazi 13kukutwa na COVID-19

Published

on

Visa vya maambukizi ya virusi vya corona vinazidi kurekodiwa kwa wingi nchini, hii ni baada ya wafanyakazi 13 wa kampuni ya Safaricom kupatikana na virusi hivyo

Kumi na tatu hao ambao wanahudumu katika duka la Safaricom kaunti ya Meru, walikuwa miongozi mwa wale waliopatikana na virusi hivyo Jumatano, Juni 17.

Katibu mkuu katika wizara ya Afya Rashid Aman amesema kuwa Safaricom imeripoti visa 14 kwa jumla vya maambukizi ya virusi vya corona baada ya mwingine mmoja kupatikana navyo Ijumaa wiki jana.

Safaricom yafunga duka lake baada ya wafanyakazi 13 kukutwa na COVID-19

Safaricom yafunga duka lake baada ya wafanyakazi 13 kukutwa na COVID-19

Kwa mujibu wa afisa wa afya kaunti ya Meru Misheck Mutuma, watu 42 waliotangamana na mgonjwa huyu wamewekwa karantini.

Kampuni ya Safaricom sasa imefunga duka lake lililoko Meru kwa muda usiojulikana baada ya visa vya COVID-19 kurekodiwa.

Comments

comments

Facebook

Trending