Connect with us

General News

Sasa yabainika Sankok anamiliki bastola mbili – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sasa yabainika Sankok anamiliki bastola mbili – Taifa Leo

Sasa yabainika Sankok anamiliki bastola mbili

NA VINCENT ACHUKA

MAAFISA wanaochunguza kifo cha mtoto wa Mbunge Maalum David Sankok anayedaiwa kujiua kwa bunduki ya baba yake, sasa wanakabiliwa na kibarua cha kubaini silaha aliyotumia baada ya kubainika kuwa mbunge huyo anamiliki bunduki mbili.

Maafisa hao Alhamisi jioni walizuru nyumbani kwa mbunge huyo katika Kaunti ya Narok na kuandikisha taarifa kwa mara nyingine kutoka kwake.

Watu 10 tayari wamerekodi taarifa kwa polisi inayosaidia maafisa wa polisi katika uchunguzi wao.Maafisa wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) Alhamisi waliendelea na uchunguzi wao maabarani kubaini ikiwa Memusi Sankok, 15, alijiua Jumatatu kwa kutumia bastola aina ya Ceska au shotgun.

Upasuaji uliofanywa Jumanne katika hospitali ya Longisa, ulithibitisha kuwa mvulana huyo alifariki kutokana na risasi iliyoingilia chini ya kidevu na kutokea utosini.

Maafisa wa uchunguzi, hata hivyo, wanasema kuwa kuna baadhi ya mambo yanayokinzana hivyo kuwalazimu kurekodi upya maelezo ya mbunge huyo.

Maafisa wa polisi walioenda katika eneo la mkasa baada ya mwanafunzi huyo wa Shule ya Upili ya Kericho kujiua kwa risasi, hawakupata ganda la risasi iliyotumika hivyo kuzua maswali zaidi.

“Hatukupata ganda lolote la risasi iliyotumika,” akasema Mkuu wa DCI tawi la Narok Mwenda Ethaiba huku akiahidi kutoa taarifa ya kina kuhusu ripoti ya uchunguzi wao.

Mvulana huyo anadaiwa kujiua ndani ya chumba cha malazi cha wazazi wake.

Ripoti ya mwanzoni, mwili ulionwa na kaka mdogo wa mwendazake ambaye baadaye alifahamisha dada yake.

Dada yake, Rosemary, 21, baadaye alifahamisha mama yao.