Connect with us

General News

Saudi Arabia yazindua uwekezaji wa Sh700 bilioni katika teknolojia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Saudi Arabia yazindua uwekezaji wa Sh700 bilioni katika teknolojia – Taifa Leo

LEAP2022: Saudi Arabia yazindua uwekezaji wa Sh700 bilioni katika teknolojia

NA FAUSTINE NGILA

Riyadh, Saudi Arabia

TAIFA la Saudi Arabia limetangaza zaidi ya Sh700 bilioni kama uwekezaji katika teknolojia na ujasiriamali wa siku zijazo ambao utaimarisha zaidi nafasi ya kuwa na uchumi mkubwa zaidi wa kidijitali katika eneo zima la Mashariki ya Kati.

Tangazo hilo lilitolewa katika kongamano la teknolojia za kisasa la LEAP 2022 ambalo linafanyika jijini Riyadh hadi Februari 3.

Uwekezaji na mipango hiyo unajumuisha uzinduzi wa hazina ya Aramco yenye thamani ya Sh110 bilioni, na uwekezaji wa kiasi sawa cha fedha kutoka kwa kampuni ya NEOM Tech, uzingativu wake ukiwa kwa teknolojia za siku zijazo.

Kama sehemu ya uwekezaji wake, NEOM ilitangaza uzinduzi wa teknolojia ya kwanza tambuzi ya metavasi duniani, ya XVRS ambayo itahudumia wakazi na wageni wa mradi wa smart giga, na M3LD, ambalo ni jukwaa la usimamizi wa data ya kibinafsi ambalo humrejeshea mtumiaji udhibiti wa data.

Kampuni ya Stc nayo ilitangaza kituo cha MENA HUB, chenye uwekezaji wa Sh110 bilioni katika muunganisho wa kikanda wa miundombinu, ambao utasaidia sekta ya kidijitali.

LEAP 2022 pia ilihusisha uzinduzi wa The Garage, jukwaa jipya la biashara changa, uwekezaji na ujasiriamali wa Chuo cha Mfalme Abdulaziz cha Sayansi na Teknolojia (KACST).

The Garage itabuni mazingira makamilifu ya kuhudumu vyema kwa wanaofanya biashara changa kitaifa na kimataifa, ili kuwasaidia kukua na kuwa kampuni zinazoongoza za teknolojia katika siku zijazo.

Kampuni ya J&T Express Group, mojawapo ya kampuni za taratibu za usafiri zinazokua kwa kasi duniani, ilitangaza uwekezaji wa Sh220 bilioni kwa ushirikiano na Kampuni ya eWTP Arabia Capital na washirika wengine.

Uwekezaji huo utaiwezesha J&T kuanzisha makao yake makuu ya MENA jijini Riyadh, na kuanzisha mtandao mpana wa taratibu zake thabiti za vifaa vya usafirishaji maarufu kama smart logistics na usambazaji ambavyo vitafungua Saudia kama kituo kikuu cha kikanda cha usafirishaji wa hali ya juu.

Saudi Arabia ndiyo soko kuu zaidi la teknolojia katika eneo la MENA, ikiwa na sekta ya teknolojia yenye thamani ya zaidi ya Sh4 trilioni.

Uwekezaji huo mpya uliotangazwa katika LEAP22 ni sehemu ya mipango inayoendelea ya Milki hiyo ya kuigeuza kuwa nchi yenye uchumi mbunifu, ambao tayari umeifanya nchi hii kuwa mojawapo ya ‘masoko’ mapya ya mambo ya teknolojia ya kifedha na kidijitali yanayokua kwa kasi zaidi katika eneo hilo.

“Uwekezaji na juhudi hizi ni dhihirisho la msukumo wa Milki hii wa kuelekea katika ukuzaji wa uchumi wa kidijitali kwa manufaa ya watu wake, sayari hii na ustawi wa eneo la MENA. Aidha, zinaashiria hatua ya ziada ya ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini Saudi Arabia, soko kubwa zaidi la teknolojia na dijitali katika eneo la MENA, “alisema Mhandisi Abdullah Alswaha, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Saudia.

Wakati wa hotuba yake kuu katika LEAP22, waziri huyo alibainisha kuwa Saudi Arabia ndiyo inayoongoza katika ukanda huo kwa vipaji vya teknolojia, ikiwa na zaidi ya ajira 318,000 katika sekta ya teknolojia katika nchi za Milki za Kiarabu, pamoja na kiwango cha ushiriki wa wanawake katika ajira za ICT, kiwango ambacho kimepanda hadi asilimia 28 katika miaka ya karibuni.

Saudi Arabia pia ni makao ya baadhi ya uwekezaji mkubwa zaidi katika teknolojia ya hifadhi ya mitandaoni, na watoa-huduma bora zinazojumuisha Google, Alibaba, Oracle na SAP ambazo zimewekeza zaidi ya Sh270 bilioni katika teknolojia hiyo.

Aramco Ventures, utanzu wa mtaji wa uwekezaji wa Saudi Aramco, ilitangaza uzinduzi rasmi wa hazina yake ya ustawi anuwai Sh110 bilioni, wa Prosperity7.

Hazina hiyo inawasaidia wajasiriamali shupavu kubuni kampuni za kuleta mabadiliko na kutatua baadhi ya matatizo magumu zaidi duniani.

Prosperity7 huzipa kampuni zake tanzu za kwingineko ufadhili na miunganisho zinaohitaji ili kujikuza na kujitosa katika masoko mapya kwa minajili ya kufikia masoko ya kimataifa.

Amin Nasser, aliye Afisa Mkuu Mtendaji wa Saudi Aramco, alisema: “Prosperity7 itafumbua mafumbo kupitia mawazo makubwa, vipaji vya juu na teknolojia za mageuzi duniani kote huku tukitazama zaidi ya upeo wa kawaida wa nguvu za thamani ya kibiashara, katika sekta kama vile afya, elimu na blokcheni, kwa suluhu za kudumu kwa matatizo makubwa zaidi duniani.”

STC

Stc ilitangaza mradi wa MENA HUB ili kuanzisha kampuni ya kujitegemea ya uwekezaji wa Sh110 bilioni bilioni katika miundombinu ya kebo za baharini na vituo vya data, ambao utaongeza hadhi ya sasa ya Saudi Arabia kama kitovu cha kidijitali cha eneo hili.

Kwa kutumia eneo la kijiografia la Saudi Arabia katikati ya ukanda wa MENA, kampuni hii itasimamia na kuendelea kuwekeza kwenye kebo za baharini zitakazojumuisha mpya zinazotua katika maeneo mbalimbali ya Saudi Arabia.

Kampuni hii itasimamia vituo vya data na kuendelea kuwekeza katika vituo vipya vya data kote nchini na katika ukanda mzima, pamoja na miundombinu mingine ya kidijitali ili kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni. Pia itataifisha matukio na kukuza huduma za cloud ili kutimiza mipango ya kidijitali ya Saudi Arabia.

Stc ilifichua ushirikiano mpya wa kimkakati na Kampuni ya Huawei Technologies, ambao utawezesha mitambo ya kutengeneza vifaa vya kituo cha data na kiwanda vikijengwa nchini Saudi Arabia, ili kuzidisha uwezo wa Saudi Arabia katika tasnia ya teknolojia ya hadhi ya juu (high tech), kuunda mkondo wa usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia na kuongeza utumiaji wa teknolojia mpya za biashara za Saudia, hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa ubunifu wa kitaifa na kuchangia katika kufikia Azimio la 2030 la Saudia.

NEOM TECH, XVRS NA M3LD

Kampuni ya NEOM Tech & Digital inayostawishwa ikiwa na kila sifa mipango ya uzinduzi wa XVRS, jukwaa la kisasa kabisa la metaverse pacha la dijitali, ambapo uhalisia kimtandao huchanganyikana na wa kawaida ili kuunda hali ya kipekee ya ukweli-mseto wa kina.

Ndiyo teknolojia pekee tambuzi ya metaverse inayoendelea kutengenezwa ikiwa na vipengele vyote katika jukwaa moja linaloweza kupanuliwa, linalounganisha mazingira halisi na ya kidijitali na kutoa fasiri ya wakati halisi na mfano wa binadamu-roboti.

XVRS ni sehemu ya uwekezaji wa US$ 1 bilioni wa Kampuni ya NEOM Tech & Digital katika teknolojia inayoendeshwa na Akili ya Kiteknolojia (AI), ambayo pia inajumuisha M3LD, jukwaa la usimamizi wa data ambalo huwapa watumiaji uwezo wa kujirejeshea udhibiti wa data zao.

“Siku zijazo zitabainishwa na miji ya meta cities. Ni maono yanayolenga uzoefu badala ya kigezo. XVRS inaweka mahitaji ya binadamu mbele- imeundwa ili kuwapa watu muda zaidi, nafasi na usalama ulioimarishwa. Wakati huo huo, M3LD, itarejesha umiliki wa data mikononi mwa watumiaji na kurejesha imani katika uchumi wa data,” Joseph Bradley, Afisa Mkuu Mtendaji wa NEOM Tech & Digital Company, alisema.

J&T na eWTP Arabia Capital

Kampuni ya J&T Express Group, mojawapo ya kampuni zinazokua kwa kasi zaidi duniani za taratibu za usafirishaji, ilitangaza uwekezaji wa US$2 bilioni Hkwa ushirikiano na eWTP Arabia Capital na washirika wengine ili kufungua makao yao makuu ya ukanda wa MENA na kujenga uwezo wa vyombo vyao vya usafirishaji na usambazaji jijini Riyadh ili kuwahudumia vyema wateja wa ndani na washirika wake.

Uwekezaji huo utajumuisha kujenga Vituo vya Uainishaji vya hadhi ya kimataifa, Mifumo ya Maghala ya Magari, Vituo vya Kusafirisha Mizigo Angani, Vituo vya Sekta ya Biashara ya Mtandaoni yaani E-commerce, na vyombo vingine vya kisasa vya viwandani na miundombinu husika, ili kutoa huduma za hali ya juu zinazoendeshwa na teknolojia kwa wateja wa J&T na washirika wake wa kibiashara.

Mheshimiwa Rais wa Mamlaka Kuu ya Usafiri wa Anga (GACA), Abdulaziz Al-Duailej, alisema kuwa miundombinu ya Vyombo na Vifaa vya Usafiri ambavyo vitaanzishwa kupitia ushirikiano huu havitakuwa tu vya kuharakisha ukuaji wa usambazaji na mizigo nchini Saudi Arabia, bali.

“Pia itaongeza eneo letu la kijiografia katikati ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ili kuifanya Saudi Arabia kuwa kituo kikuu cha huduma za vyombo vya usafiri wa hali ya juu.”

“Katika miaka 10 ijayo, kwa ushirikiano na eWTP Arabia Capital na washirika wengine wa kimkakati, J&T itawekeza katika vifaa na programu za kidijitali za hali ya juu nchini Saudi Arabia, kutoa mafunzo kwa vikosi bora zaidi vyya wataalamu, kujenga kiwanda kikubwa zaidi cha vyombo vipevu zaidi vya usafiri katika ukanda wa MENA , kuhudumia soko zima la ukanda huu, na kukuza maendeleo ya kina ya uchumi wa kitaifa wa viwanda unaoendeshwa na teknolojia,” alisema Jet Lee, Mwanzilishi aliye pia Mwenyekiti wa Kundi la J&T Express.

The Garage: Eneo la Biashara Changa

KACST ilitangaza ‘The Garage: Eneo la Biashara Changa’, mchanganyiko wa eneo halisi, inkyubeta ya biashara changa, kichochezi na mengi mengineyo, ambayo yatazipa biashara changa zinazoanzishwa ufadhili wa ruzuku, uwekezaji,matangazo ya masokoni na mafunzo, nafasi za kazi kwa huduma kamilifu.

Itawezesha wamiliki wazo kufikia maabara za teknolojia ya kina, vipaji na mitandao ya utafiti, miongoni mwa motisha nyinginezo za kuwawezesha waanzishaji wa biashara hizo wa humu nchini na kimataifa kujikuza ili kuwa kampuni zinazoongoza za teknolojia siku zijazo.

The Garage inalenga kuzindua biashara changa zinazoanzishwa kwa uwezo wa kitaifa na kimataifa.

“The Garage imechochewa na mwanzo mdogo wa baadhi ya kampuni kubwa katika teknolojia leo hii, na inalenga kuzipa kila kitu ambacho zinahitaji ili kukuza maoni yazo, kuwa kampuni kubwa za teknolojia kimataifa. Inapatikana mahali pazuri karibu na nyenzo au miundombinu ya kisasa na kwenye idadi kubwa ya talanta inayounda mazingira bora ya eneo la biashara changa zinazoanza,” alisema Dkt Munir Eldesouki, Rais wa KACST na mkuu wa kikosi anzilishi cha Mamlaka ya Utafiti, Maendeleo na Ubunifu.

PASPOTI YA BIASHARA CHANGA

Shirika la Digital Cooperation (DCO), likiwa shirika la kimataifa lililoanzishwa ili kuwezesha ustawi wa kidijitali kwa wote, leo limetangaza uzinduzi wa Paspoti ya Biashara Changa ya DCO ili kurahisisha na kupunguza gharama kwa wanaoanza kufanya biashara nje ya mipaka, hali itakayofungua na kuongeza masoko yanayoweza kuleta faida kubwa kwa watu wanaozidi nusu bilioni.

“Paspoti ya Biashara Changa zinazoanzishwa inapunguza vikwazo vya kiutawala na kifedha na kuongeza kasi ya usajili wa mashirika na michakato mingine kwa wajasiriamali. Kupitia paspoti hii, wataweza kuingia katika masoko ya nchi nyingine wanachama wa DCO. Hii itaendeleza dhamira yetu ya kuratibu juhudi na kubadilishana utaalamu ili kukuza uchumi wa kidijitali kwa manufaa ya mataifa yote,” Deema Al-Yahya, Katibu Mkuu wa DCO alisema.

Paspoti ya Biashara Changa zinazoanza inawezesha uingiaji na usaidizi wa haraka katika masoko ya nchi nane za DCO. Mpango huo utazinduliwa kwanza nchini Saudi Arabia na Nigeria.

Wakati wa LEAP 22, DCO pia iliidhinisha Elevate50, mpango uliozinduliwa ili kusaidia biashara 50,000 ndogondogo na za hadhi ya kati kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kuuza bidhaa zao mtandaoni. Ikiungwa mkono na jukwaa la biashara ya mtandaoni la Jordan la MakanE, Elevate50 inakadiriwa kuzalisha nafasi za kazi 5,000 na inalenga hasa biashara zinazoendeshwa na wanawake na vijana.

Makala ya kwanza ya LEAP yanatazamiwa kuwa jukwaa kubwa zaidi la teknolojia. Itaangazia mfumo mzima wa uvumbuzi, ikiunganisha waanzilishi na wanamageuzi kibiashara na viongozi wa serikali, wajasiriamali, wawekezaji na wengineo zaidi ili kupata uzoefu na kujifunza kuhusu teknolojia za siku zijazo.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending