Msemaji wa Seneta huyo, Alex Kiprotich alithibithishia shirika moja la habari kuwa tayari Moi aliwasili nchini Malawi kumwakilisha Rais Uhuru Kenyatta.
Ikulu pia ilifichua hotuba ya Uhuru ambayo Moi atasoma kwa niaba yake.
Katika hali ya kawaida, Naibu Rais William Ruto ndiye alitakiwa kumwakilisha rais katika hafla kubwa kama hiyo.
Tangia mwaka jana, amekuwa akiwachagua viongozi wengine kumwakilisha katika hafla za michango ambapo pia Ruto amekuwa akihudhuria.
Mbunge wa Nyeri Mjini, Ngunjiri Wambugu alisema Uhuru alikuwa akiwachagua viongozi wengine badala ya Ruto kwa sababu hana imani naye.
Uhusiano wa wawili hao umekuwa na doa tangia maridhiano ya Machi 2018.
Chakwera alipata 58.57% ya kura zilizopigwa Jumanne, Juni 23, wakati uchaguzi wa Malawi ulikuwa unarejelewa baada ya kufaulu kupinga ushindi wa aliyekuwa rais Peter Mutharika kortini.
Mnamo Februari 2020, korti hiyo iliamua kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mei 2019, ulikumbwa na udanganyifu na hivyo kuelekeza uchaguzi huo uandaliwe upya.
Taarifa kutoka Malawi imefichua kuwa hafla hiyo itahudhuriwa na watu 100 pekee kwa mintarafu ya janga la COVID-19.