Seneta Sakaja alala ndani baada ya kunaswa akibugia pombe usiku. Source: UGC
Taarifa iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Kilimani ilionesha watu wengine saba waliokuwa wakijivinjari na seneta huyo katika baa ya Lady’s Lounge kwenye barabara ya Dennis Pritt walihepa mtego wa polisi.
Maafisa waliofika eneo ambalo kumi hao walikuwa wakijivinjari walimuagiza seneta huyo kuondoka lakini alidinda na kuwalazimu kuwajulisha wakubwa wao kuhusu tukio hilo.
Naibu kamanda wa eneo la Kilimani Adan Hassan alikuwa miongoni mwa maafisa wakuu waliofika ndani ya baa hiyo kumshurutisha Sakaja kuondoka lakini alipokuwa mkaidi hawakuwa na budi ila kumfunga pingu.
Seneta Sakaja alilala katika kituo cha polisi cha Kilimani. Source: UGC
Hata hivyo, aliachiliwa huru lakini akadinda kuondoka kituoni huku akitishia kuwapa uhamisho maafisa wote waliomkamata katika muda wa saa 24.
Hatimaye aliondoka kizuizini.
Mnamo Julai 6, 2020 Rais Uhuru Kenyatta alitangaza amri ya kufungwa kwa baa xote nz maeneo ya burudani kwa siku 30 zaidi wakati taifa linapoendelea kukabiliana na COVID-19.